Misaada ya Kujifunza
26. Kaisaria Filipi


26. Kaisaria Filipi

picha 26

Kaisaria Filipi iko mguuni mwa Mlima Hermoni. Chemchemi hii ni moja ya vyanzo vya Mto Yordani. Herode Filipo, ambaye alitawala eneo hili, alijenga mji hapa kwa heshima ya Kaisari (mfalme wake) na yeye mwenyewe; awali mji huu uliitwa Pania na leo unaitwa Baniasi vile vile Kaisaria Filipi.

Matukio Muhimu: Mwokozi alikutana pamoja na wanafunzi Wake katika Kaisaria Filipi. Hapa ndipo Petro alipotamka kwamba Mwokozi alikuwa “ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai”. Kisha Mwokozi akamwahidi Petro “funguo za ufalme wa mbingu” (Mt. 16:13–20).