Misaada ya Kujifunza
30. Korintho


30. Korintho

picha 30

Korintho ulikuwa mji mkuu wa jimbo la Kirumi la Akaya. Ulikuwa uko juu ya shingo ya nchi iunganishayo Peloponeo pamoja na nchi ya bara la Uyunani, ukimiliki bandari pande zote mashariki na magharibi. Ulikuwa mji wa bandari ya utajiri na umashuhuri.

Matukio Muhimu: Paulo aliishi katika Korintho kwa mwaka mmoja na miezi sita na akalianzisha Kanisa hapa (Mdo. 18:1–18). Paulo aliandika barua kadhaa kwa waumini wa Kanisa katika eneo la Korintho, mbili kati ya hizo sasa zimo katika Agano Jipya (1 na 2 Wakorintho). Waraka kwa Warumi yawezekana sana kuwa uliandikwa kutoka Korintho.