2. Mlima Sinai (Horebu) na Nyika za Sinai
Kuna maeneo kadhaa yanayowezekana kuwa ndiyo mahali pa Mlima Sinai. Moja ya maeneo ya kimapokeo ni Yebeli Musa (Mlima wa Musa), uliopigwa picha hapa.
Matukio Muhimu: Mungu alimtokea Musa na akampa Amri Kumi (Ku. 19–20). Musa, Haruni, wana wawili wa Haruni, na wazee 70 walimwona na kuzungumza na Mungu (Ku. 24:9–12). Mungu alimpa Musa maelekezo kwa ajili ya kujenga hema (Ku. 25–28; 30–31). Waisraeli walimwabudu ndama wa dhahabu ambaye walimshawishi Haruni kumtengeneza (Ku. 32:1–8). Eliya alikimbilia katika nchi hii kutoka Bonde la Yereezeli, mahali ambapo Malkia Yezebeli aliishi (1 Fal. 19:1–18). Hapa ni mahali ambapo pia Eliya alizungumza na Mungu (1 Fal. 19:8–19). (Ona MWM Sinai, Mlima.)