3. Nyika za Uyahudi
Nyika za Uyahudi ziko mashariki mwa Yerusalemu na hushuka hadi Bahari ya Chumvi.
Matukio Muhimu: Nyika za Uyahudi zilikuwa ni kimbilio muhimu katika nyakati nyingi za historia ya awali. Daudi alijificha asionekane na Mfalme Sauli (1 Sam. 26:1–3). Yesu alifunga kwa siku 40 mchana na 40 usiku (Mt. 4:1–11; Mk. 1:12–13). Yesu alitumia njia hii kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko kupitia nyika za Uyahudi kama mandhari kwa ajili ya mfano wa Msamaria mwema kwa sababu waliokuwa wakisafiri peke yao walikuwa wakishambuliwa kwa urahisi katika eneo lile (Lk. 10:25–37). (Ona MWM Bahari ya Chumvi.)