Misaada ya Kujifunza
8. Yerusalemu


8. Yerusalemu

picha 8

Ukiangalia upande wa kaskazini juu ya Yerusalemu. Katikati ya picha ni madhabahu ya Kiislamu yenye kuba iliyofunikwa kwa dhahabu, inayoitwa Kuba ya Mwamba. Wayahudi hapo kale walifanya ibada katika hekalu lililokuwa hapa. Kuta karibu na Kuba ya Mwamba huuzunguka mji wa zamani wa Yerusalemu. Kulia kwa ukuta ni Bonde la Kidroni. Mbali kulia ni Mlima wa Mizeituni. Kwa kaskazini kuvuka Kuba ya Mwamba, yawezekana kuwa ni eneo la Golgotha, au Kalivari.

Matukio Muhimu: Hapo kale Yerusalemu ilikuwa ikiitwa Salemu (Zab. 76:2). Ibrahimu alilipa zaka kwa Melkizedeki (Mwa. 14:18–20). Ibrahimu akaja kumtoa dhabihu Isaka (Mwa. 22:2–14). Mfalme Daudi aliiteka Yerusalemu kutoka kwa Wayebusi (2 Sam. 5:4–9). Mfalme Sulemani alijenga hekalu (1 Fal. 6–7). Lehi aliondoka kwenda nchi ya ahadi (1 Ne. 1:4; 2). Mwokozi alihudumu, alilipia dhambi zetu, na alifufuka (Mt. 21–28). Kama Mwokozi alivyotoa unabii, Yerusalemu iliangamizwa muda mfupi baada ya kifo Chake (JS—M 1:3–20). Yerusalemu itavamiwa katika siku za mwisho (Eze. 38–39; Yoe. 2–3; Ufu. 11; 16). Mwokozi ataonekana hapa kama sehemu ya Ujio Wake wa Pili (Zek. 12–14; M&M 45:48–53). (Ona MWM Yerusalemu; Salemu.)