22. Mlima Tabori
Picha
picha 22
Ukiangalia Kaskazinimagharibi kuelekea Mlima Tabori. Nyanda za chini zinazouzunguka Mlima Tabori ni sehemu ya Bonde la Yezereeli. Nazareti inalala katika vilima vilivyo jirani na Mlima Tabori.
Matukio Muhimu: Debora na Baraka walikusanya majeshi ya Bwana dhidi ya Yabini, Mfalme wa Hazori (Amu. 4:4–14). Mlima Tabori ni moja ya maeneo ya kimapokeo ya Kugeuka Sura kwa Mwokozi (Mt. 17:1–9); mwingine ni Mlima Hermoni. (Ona MWM Kugeuka sura.)