Misaada ya Kujifunza
9. Hekalu la Herode


9. Hekalu la Herode

picha 9

Picha hii huonyesha mfano wa vipimo vya hekalu la Herode (skeli ya uwiano 1:50) kama ilivyofikiriwa kuwa katika mwaka 67 B.K. Ukuta unaozunguka majengo ya hekalu huzizunguka sehemu takatifu zenye kujumuisha patakatifu pa patakatifu, mahali patakatifu, na mabehewa makuu matatu.

Matukio Muhimu: Yusufu na Maria walimleta mtoto mchanga Yesu hekaluni (Lk. 2:22–38). Mwokozi alifundisha hekaluni akiwa na umri wa miaka 12 (Lk. 2:41–46). Mwokozi aliwafukuza wabadilisha fedha kutoka hekaluni (Mt. 21:12–13) na akatabiri angamizo la hekalu (Mt. 24:1–2). Hekalu la siku za baadaye litajengwa katika Yerusalemu (Eze. 40–48; Zek. 8:7–9). (Ona MWM Hekalu, Nyumba ya Bwana.)