“Sehemu ya Burudani,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2022.
Sehemu ya Burudani
Maelezo Shindano
Picha hii inahitaji kipaji chako cha ucheshi! Tutumie barua pepe nukuu yako bora (ifikapo Julai 31) kwenda ftsoy@ChurchofJesusChrist.org. Lakini kwanza, hakikisha na usome maingizo unayopenda kutoka kwa shindano la mwisho (lililochapishwa Agosti 2021).
-
Akina dada wanaohudumu sana: “Je, mlipata biskuti tulizowaachia?” Jordan J.
-
“Je, hapa ndipo palipo na karamu ya Chihuahua? Firulais alinialika.” Jeanett V.
-
“Inatia aibu. Usimwambie paka kilichotokea.” Silvia S.
-
Unaposikia mtu akisema jina lako kwenye mazungumzo. Rochelle K.
-
Ni wakati gani mleta barua atakuja Kwa Nguvu ya Vijana. Betty J.
-
“Nasikia harufu ya Bacon!!!” Ken C.
-
Ukiwa na swali lakini mama yako ana hasira. Emerie K.
-
Ni rahisi zaidi kwa mbwa-mwitu kupita kwenye mlango wa paka kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu” (ona Mathayo 19:23). Ainsley L.
-
Yote safi. Washa operesheni ya “Ingia kwenye Ghala la Chakula cha Mbwa.” Grace L.
-
Watoto wa msingi wakichungulia Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama wanapotoka darasani mapema. Brynn M.
-
“Nitakuwa nikitazama kila wakati.” Braeden D.
-
Kujaribu kutotazamana macho wakati mwalimu anauliza, “Nani anataka kusema sala ya kufunga?” Benson S.
-
Unapojaribu kujibana ndani ya shati lako unalolipenda kutoka darasa la tatu. Paisley S.
-
Lehi: “Tunaenda kwenye nchi ya ahadi.” Mbwa: “Naweza kuja?” Noah P.
Mtumaini Mungu
Katika chamsha bongo ya kawaida ya Sudoku, lengo lako ni kujaza gridi ya 9x9 ili kila safu, kila rafu, na kila moja ya visanduku tisa vya 3x3 vitumie tarakimu kutoka 1 hadi 9 mara moja tu. Wakati huu, hata hivyo, tumia maneno tisa yafuatayo badala ya tarakimu. Maneno haya yote yanahusiana na kujifunza kumwamini Mungu.
Subira
Sala
Utiifu
Imani
Moyo
Hisani
Huduma
Unyenyekevu
Shukrani
Vichekesho
Majibu
Mtumainie Mungu (Sudoku).