“Usiogope, Bwana Yu pamoja Nawe,” Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2022.
Neno la Mwisho
Usiogope—Bwana Yu pamoja Nawe
Kutoka kwenye hotuba ya mkutano mkuu wa Oktoba 2018.
Hofu si ngeni. Kuanzia nyakati za kale, woga umedhibiti mtazamo wa watoto wa Mungu. Katika 2 Wafalme, mfalme wa Shamu alikuwa ametuma jeshi kumkamata na kumuua nabii Elisha.
“Na wakati mtumishi wa [Elisha], alipoamka asubuhi na mapema, na kwenda nje, tazama wamezingira jiji na jeshi la watu, na farasi na magari.” Na mtumishi wa [Elisha] kijana akamwambia, Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje?” (2 Wafalme 6:15).
Hii ilikuwa hofu ikizungumza.
“Na [Elisha] akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.
“Na Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.”(2 Wafalme 6:16–17).
Twaweza au hatuwezi kutumiwa magari ya moto kuondoa hofu zetu na kushinda mashetani wetu, lakini somo ni bayana. Bwana yu pamoja nasi, anatujali na anatubariki katika njia ambazo ni Yeye tu Anayeweza kufanya hivyo.
Kama tutamtumainia Bwana na njia Zake, kama tutashiriki katika kazi Yake, hatutaogopa mitindo ya dunia au kutishwa nayo. Bwana anatuangalia, anatutunza, na anasimama karibu nasi.