2022
Ungana
Julai 2022


“Ungana,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2022

Ungana

Ana Julia A.

17, São Paulo, Brazil

Picha
msichana

Picha na Leonardo Conceição Motta

Ninaishi katika eneo lenye watu wengi zaidi katika nchi yangu. Ninapenda kuishi hapa na kugundua maeneo mapya na familia yangu. Ninaishi na wazazi wangu, dada yangu mdogo, na mbwa wetu, Meghan. Ninapenda kuwa pamoja nao. Tunacheka sana na kujaribu kufanya mambo mapya na ya kuvutia. Tunapenda baadhi ya vitu fulani bora kuliko vingine, lakini uzoefu hukaa nasi milele.

Niko katika mwaka wangu wa mwisho wa shule, na ninajiandaa kwa mitihani ya mwisho. Nina wasiwasi kidogo, lakini ninatumaini Bwana atanisaidia kupitia hayo.

Ninapenda kwenda kanisani kila Jumapili. Kuna vijana wengi katika kata yangu, hivyo shughuli ni za kufurahisha. Vijana wanaonizunguka hunisaidia kukaa imara katika injili. Naweza kusema wana imani sana.

Ninajiandaa kutumikia misheni. Ninataka kushiriki injili na wengine kama wamisionari walivyofanya na familia yangu. Najua itabadilisha maisha yao na yangu milele. Ninashukuru kujua kwamba ninaweza kuwa na familia ya milele.

Chapisha