2022
Kwa nini hakuna miujiza leo kama ilivyo katika maandiko?
Julai 2022


“Kwa nini hakuna miujiza leo kama ilivyo katika maandiko?” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2022.

Kwenye Hoja

Kwa nini hakuna miujiza leo kama ilivyo katika maandiko?

Picha
kipofu akiponywa na Yesu

Maandiko yana simulizi nyingi za miujiza. Baadhi ni kubwa na ya kuvutia, kama kugawanya Bahari ya Shamu au kumfufua mtu kutoka kwa wafu. Lakini vipi kuhusu leo? Je, miujiza bado hutokea?

Ndio, inatokea. Hatuwezi kusikia juu yao kila wakati, lakini miujiza bado inatokea katika maisha ya watu kila wakati.

Mzee Ronald A. Rasband wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili amesema: “Wengi wenu mmeshuhudia miujiza, zaidi ya mnavyotambua. Inaweza kuoneka midogo. … Lakini ukubwa hautofautishi muujiza, ila kwamba tu ulitoka kwa Mungu” (Aprili 2021 mkutano mkuu [Liahona, Mei 2021, 110]).

Msaada wowote kutoka kwa Mungu unaweza kuitwa muujiza. Watu wengi hupata miujiza. Watu hao wakati mwingine hushiriki hadithi zao, lakini mara nyingi wanaziweka kuwa takatifu—kati yao wenyewe na Mungu.

Na kumbuka mambo haya mawili muhimu kuhusu miujiza: (1) miujiza huja tu kama watu wanayo imani, na (2) miujiza hutokea kulingana na mapenzi ya Bwana na wakati. Huenda tusipate kuchagua jinsi gani au lini, lakini miujiza ya Bwana hutokea, hata leo. Hata kwako

Chapisha