2022
Nitaamuaje wakati ulio bora kwenda kutumikia misheni?
Julai 2022


“Nitaamuaje wakati ulio bora kwenda kutumikia misheni?,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2022.

Maswali na Majibu

“Nitaamuaje wakati ulio bora kwenda?”

Bwana Huandaa Njia

msichana

Baba yetu wa Mbinguni ana kazi ya kufanya kwa ajili yetu. Tunaposoma maneno Yake, na maneno ya watumishi Wake waliochaguliwa, tunaweza kujua kwa ujasiri kile ambacho angetaka tufanye. Tunajua Bwana atatutayarishia njia tuweze kutimiza mambo Anayotuomba tufanye (ona 1 Nefi 3:7). Atakuwa daima kwa ajili yetu ikiwa tunajitahidi kutii amri Zake.”

Manuela O., 15, Ghana

Huenda Usijisikie Tayari 100%

mvulana

Mimi ni mtaalamu wa kuteleza kwenye mawimbi, na ninasitisha hilo ili kupata uzoefu wa furaha ya kweli inayotokana na kutumikia misheni. Nilingoja hadi nilipohisi kuwa nilikuwa tayari kweli kwenda, na nimebarikiwa kwa hilo. Ni uamuzi kati yako na Baba yako wa Mbinguni. Huenda usijisikie tayari 100%. Kuwasilisha karatasi zako za misheni daima kutakuwa imani kubwa, lakini inafaa sana.

Jordan C., 22, California, Marekani

Bwana Atakuandaa na Kukutia Nguvu

“Unaweza kumwomba Bwana kila wakati katika maombi. Bwana huwawezesha wale anaowaita kuwa wamisionari. Baba yangu alipokufa, nilifarijiwa na ushuhuda wangu wa mpango wa wokovu. Lakini kuna watu wengi katika ulimwengu huu ambao bado hawajui kuhusu mpango wa Baba wa Mbinguni. Ninajua Bwana anatayarisha watu kwa ajili yangu kuwafundisha.”

Felipe F., 17, Brazili

Andika Misukumo

msichana

“Nilipoomba kuhusu kutumikia misheni, niliandika misukumo niliyopokea kutoka kwa mazungumzo, muziki, au marafiki. Nilipohisi kuvunjika moyo nilipokuwa nikijiandaa kwa misheni yangu, nilirudi nyuma na kusoma mambo ambayo Roho alikuwa ameniambia. Niliwasilisha karatasi zangu na kumwamini Bwana. Unaposonga mbele kwa imani, hujui jinsi itakavyokuwa, lakini utaona mkono wa Mungu katika kufanya maamuzi yako!”

Bryanna M., 19, Oregon, Marekani

Pokea Baraka Yako ya Kipatriaki

msichana

“Tangu nilipopokea baraka zangu za patriaki, nimejua kwamba nilipaswa kushiriki injili. Ninajiandaa kwa misheni sasa kwa kushiriki injili na marafiki zangu. Hata kama ninahisi kwamba kutumikia misheni ya muda wote sio sawa kwangu ninapokuwa mkubwa, bado najua kwamba ninaweza kushiriki injili maisha yangu yote.

Elise D., 14, Florida, Marekani

Muulize Bwana na Wengine

“Ninaweza kuwa na umri wa miaka 14 tu, lakini nimekuwa nikitafakari swali hili mwenyewe. Wakati utakapofika wa mimi kuamua ni lini ninafaa kutumika, nitaomba kwa Bwana anisaidie kupata jibu langu. Pia nitazungumza na watu walio karibu nami zaidi, ikiwa ni pamoja na familia yangu, askofu, na marafiki.”

Jordan V., 14, Nevada, Marekani

Bwana Atakupa Jibu

“Siku zote nimekuwa na hamu ya kutumikia misheni, lakini najua sio uamuzi rahisi. Ikiwa tutatafuta kwa bidii kusoma maandiko na kuomba daima kwa Baba wa Mbinguni, najua atatuongoza. Mtumaini Bwana. Atakuambia wakati unaofaa kwako kutumikia misheni. Endelea kutafuta jibu, na utalipokea na utajihisi uko tayari.”

Nicolle R., 14, Brazili

Jiandae Kiroho, Kiakili, na Kimwili

Omba kwa uaminifu na utafakari maandiko kuhusu uamuzi wako. Kuwa tayari kwa yale ambayo Roho anaweza kunong’ona au kukuambia. Na kwa wakati huu, unaweza kuhudhuria mikutano yote ya sakramenti, seminari, madarasa ya shule ya Jumapili, na madarasa ya Wasichana au mikutano ya akidi ya Ukuhani wa Haruni. Unaweza pia kujiandaa kiakili na kimwili.”

Addison H., 14, Utah, Marekani