Majasiri wa Agano la Kale
Esta Alikuwa Shupavu
Esta likuwa ni malkia wa Uajemi. Mfalme hakujua kwamba Esta alikuwa ni Myahudi. Mfalme alikuwa na rafiki mwovu aliyewachukia Wayahudi. Alimdanganya mfalme kutangaza kwamba Wayahudi wote katika nchi lazima wauwawe. Esta aliamua kumwomba mfalme awaokoe watu wake. Lakini angeweza kuuwawa kwa kwenda kwenye kiti cha enzi cha mfalme. Esta aliwaomba Wayahudi wafunge kwa ajili yake. Wakati Esta alipokwenda kwenye kiti cha enzi cha mume wake, alikaribishwa. Alimwalika mfalme pamoja na rafiki zake kwenye karamu. Hapo, aliwaambia kwamba yeye ni Myahudi. Mfalme hakuweza kubadilisha sheria, lakini aliwaruhusu Wayahudi kujilinda wao wenyewe. Kwa msaada wa Mungu, Esta aliwaokoa watu wake!
Esta
Esta alikuwa jasiri na alimwamini Mungu. Ninaweza kuwa shupavu na kusimamia kilicho sahihi!
-
Kariri sehemu ya mwisho ya Esta 4:14.
-
Angalia video ya sura ya 45 ya hadithi za Agano la Kale toka scripturestories.lds.org.
-
Kama wazazi wako wanasema umekuwa vya kutosha, funga kwa ajili ya mtu fulani unayemjali.
-
Ninaweza kuwa shupavu kwa …