2018
Michael Isaac—Bydgoszcz, Poland
Oktoba 2018


Taswira za Imani

Michael Isaac

Bydgoszcz, Poland

“Ugonjwa unaweza kufanya mambo mengi mazuri,” anasema Michael, ambaye figo yake haifanyi kazi. Kwa sababu ugonjwa wake umeongeza shukrani yake kwenye injili, anasema, “ni jaribu zuri.”

Leslie Nilsson, Mpiga picha

Michael Isaac

Nilizaliwa huko Ethiopia mwaka 1942 na kwenda Poland kusoma mwaka 1965. Mwaka 1991, nilikutana na wamisonari na kujiunga na Kanisa. Nimekwisha hudumu kama rais wa tawi kwa miaka mitatu na nusu. Nilihudumu kama mshauri katika urais wa misheni kwa miaka 12. Nilikuwa rais wa tawi tena na kisha rais wa wilaya. Kisha niliugua kutokana na figo kushindwa kufanya kazi.

Sasa ninaweza kufanya vitu vichache tu Kanisani. Ninajaribu kuhudhuria Jumapili.

Mwanzoni nilikuwa na hasira.

“Kwa nini mimi?” Nilisali. “Nimekutumikia, Bwana.” Baada ya muda, nilielewa. Maandiko yanasema, “yule aliye na imani kwangu ya kuponywa, na hakuteuliwa kufa, ataponywa” (M&M 42:48).

Mstari huu unasema tutaponywa kama hatukuteuliwa kufa.

Waumini wa Kanisa wanaendelea kuniombea, lakini afya yangu inazorota zaidi. Wanafikiri sala zao hazisikilizwi, lakini zinasikilizwa kwa sababu wanakuwa watu wazuri zaidi na kwa sababu ninahisi upendo wanaonionyesha.

Hata kama ningekuwa mwenye afya, ni muda gani ungekuwa umebakia katika umri wangu? Bado, mengi yako mbele yangu.

Ninapenda kwenda kwenye maandiko na kuona mashujaa ambao wananisaidia. Nilipokuwa mwenye afya na nikihudumia, nilipenda kumfuata Nefi, lakini sasa mara nyingi namfikiria Ayubu. Alikuwa ni mtu mzuri, na aliteseka pia. Kuna tumaini mara zote katika injili.

Katika jiji kama Bydgoszcz, kama ninataka kumtembelea meya, sitaweza kuwa na fursa kwa sababu mimi ni mdogo sana katika hilo. Lakini kupitia injili, mara zote mlango u wazi kwa ajili ya kumuita Mungu. Hii ndiyo sababu nalipenda kanisa langu.

Nina kanisa. Nina njia ya kuwasiliana na Mungu kupitia sala, kupitia kufunga, kupitia vitu vyote tufanyavyo. Je, nahitaji nini kingine?

Wakati mwingine najiambia nafsini mwangu, “Labda ndio maana ninaumwa—ili kwamba ningeweza kuelewa niko katika jambo kuu kiasi gani, hii ni sababu kuu kiasi gani.”

Ninamuona mke wangu, Renata, akiwa na huzuni kwa sababu ninaumwa. Nisingependa hii itokee, lakini huzuni ni sehemu ya upendo. Kama asingenipenda, asingekuwa na huzuni. Upendo hukusaidia kuhisi kuwa hauko peke yako na kwamba kuna watu wanaokujali.

Kufa si kitu. Kila mtu atakufa. Inategemea ni kwa jinsi gani tunakichukulia kifo. Ninajua kwamba Mungu anaishi. Anatupenda sote—ikijumuisha mimi pia. Haya ndiyo ninayoweza kusema.

Michael sitting with his wife

Kuumwa kwa Michael kumekuwa ni wakati mgumu kwa mke wake, Renata. “Ninamuona mke wangu akiwa mwenye huzuni kwa sababu ninaumwa,” anasema. “Lakini huzuni ni sehemu ya upendo. Upendo hukusaidia kuhisi kuwa hauko peke yako na kwamba kuna watu wanaokujali.”

Michael talking to a man at church

Bila kujali ukomo unaosababishwa na ugonjwa wake, Michael bado hutafuta njia za kutumikia na kuwainua wale wanaomzunguka.

Michael sitting at church

Michael hupata tumaini na mwongozo katika maandiko. Alipokuwa mwenye afya na akihudumia, alimpenda Nefi. “Lakini sasa mara nyingi ninamfikiria Ayubu,” anasema. “Alikuwa ni mtu mzuri, na aliteseka pia.”