2018
Kile ambacho Kila Askofu Hutaka Waumini wa Kata Yake Wajue.”
Oktoba 2018


Kile ambacho Kila Askofu Hutaka Waumini wa Kata Yake Wajue

Mwandishi anaishi Utah, Marekani.

Hizi ni kweli nane nilizojifunza wakati nikihudumia kama askofu.

Nilikuwa na fursa nzuri ya kuhudumia kama askofu. Katika miaka hiyo, nilijifunza masomo zaidi ambayo yanaweza kuorodheshwa. Lakini nilijifunza kweli nane ambazo naamini ziko kote. Wakati hii si orodha ya yote, ni nia yangu kushiriki kile ambacho kila askofu hutumaini waumini wa kata yake wajue.

1. Askofu humpenda kila muumini wa kata yake katika njia ya kweli.

family

Upendo alionao askofu kwa kata yake umeunganishwa kwenye upendo ambao Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanao kwa kila mmoja wetu. Wakati askofu akiwaangalia waumini wakati wa mkutano wa sakramenti, huruma na uelewa wa hali zao huja juu yake katika njia ambayo haifanani na chochote ambacho amewahi kupitia. Wakati askofu akisimama na kushiriki jinsi gani anavyowapenda waumini wa kata yake, hisia zake ni za dhati na za kweli. Jua kwamba askofu wako anakupenda, ana wasiwasi juu yako, na anakujali zaidi ya unavyofikiria.

2. Askofu husaidiwa kimwili, kihisia, na kiroho kwa imani na sala za waumini.

man standing at the pulpit

Askofu hutumia saa nyingi zisizohesabika katika kuhudumia. Mara nyingi atatumia saa nyingi kanisani Jumapili na wiki za nyongeza usiku baada ya kazi ya kutembelea, kufanya usaili na kuwatunza waumini wa kata yake.

Askofu anaweza kufanya hivi wiki hadi wiki kwa sababu ya imani na sala za waumini wa kata. Kama askofu mpya niliyeitwa, machozi bila kutaka yalitiririka kila mara niliposikia muumini akisali kwamba “mbariki askofu wetu.” Sala zenu za imani kweli hujibiwa, na askofu hupokea na kuhisi ushawishi endelevu wa sala hizo. Bwana hujibu sala hizo zilizojaa imani kwa maaskofu wa Kanisa.

3. Askofu mara nyingi huhisi kutofaa kwa ajili ya wito (hata baada ya miaka mitatu au minne).

man with head in his hands

Ninawajua maaskofu wachache ambao walihisi walikuwa “wameandaliwa” kwa ajili ya wito. Hata hivyo, ninajua, kwamba “Aitwaye na Bwana, Bwana humstahilisha.”1 Wakati askofu akijua anaelekea ustahiki, pia hutatizwa na hisia za kuona kwamba hataweza kutimiza wito vizuri. Atafanya awezavyo kutoa ushauri wa busara wakati ukihitajika, kutowaudhi watu, na kuwa kwenye hali ya kuwa na Roho, lakini bado atakuwa na wasiwasi wakati mwingine kama anatimiza wito wake inavyokubalika.

4. Roho wa Mungu anaweza kufanya kazi kupitia askofu wakati akishauriana na waumini wa kata.

two men talking

Ninapoulizwa ni nini ninakikosa zaidi kuhusu kuhudumia kama askofu, ninawaambia watu kwamba nakosa ushawishi wa nguvu wa Roho ambao huandamana na joho la askofu. Iwe ni katika kuwafariji wale ambao wamepoteza wapendwa, kuongea na wale wanaotatizwa na wenzi wasio waaminifu, au kuwaita watu kwenye toba, Roho ambaye hupatikana kwa askofu mwaminifu ni Roho wa Mungu na roho ya ufunuo.

Hivi karibuni niliombwa msaada na muumini ambaye alikuwa wa kata yangu kumsaidia kushughulikia matatizo binafsi. Alikuwa amehamia kwenye kata mpya na hakuwa na uhakika kama alitaka kwenda kwa askofu wake mpya kwa ajili ya mwongozo. Nilishiriki pamoja naye kile ambacho nimeshiriki mara nyingi tangu nilipopumzishwa, ambacho kilikuwa ni kwamba japo ningependa kusaidia, sishikilii tena funguo ambazo askofu anashikilia na kwamba funguo hizo zingekuwa muhimu kutoa msaada aliouhitaji. Nilipendekeza kwamba aongee na askofu wake. Nilimtembelea wiki mbili baadae, na akasema kwamba alikutana na askofu wake na ilikuwa kama vile tayari alikuwa ameshajua matatizo yake yalikuwa ni yapi na jinsi ya kumsaidia vizuri zaidi. Wakati askofu akiwa si mkamilifu, Bwana humpa mwongozo wa kiungu, humwongoza, na hubariki maisha kupitia maneno yake.

5. Askofu ni mwanadamu; wakati mwingine hufanya makosa na wakati mwingine hufanya vitu visivyotakiwa.

man falling

Maaskofu, hata hivyo, ni wanadamu wenye kufa. Wana mapungufu, udhaifu, upendeleo, na matatizo yao binafsi. Roho humstahilisha mtu ambaye anashikilia ofisi ya askofu, lakini askofu bado ni mtu ambaye hajakingwa dhidi ya matatizo na udhaifu sawa na ule ambao sote tunakumbana nao.

Utambuzi huu hautakiwi kupunguza heshima tunayoonyesha katika wito wake au mwitikio tunaotoa kwa ushauri wake. Askofu anatambua vyema udhaifu wake na anajitahidi kuushinda au angalau kuuweka kando ya huduma yake kama askofu. Hata kwa kujaribu sana namna gani, mara zote hatakuwa mkamilifu.

6. Askofu huhisi kwamba hawezi kamwe kuwaona waumini wa kata vya kutosha au kufanya vizuri kiasi cha kutosha.

people talking

Kila siku askofu humfikiria nani mwingine angeweza au anapaswa kumsaidia siku hiyo. Ningependa kumtembelea kila muumini mara kwa mara, lakini nilikuwa na kazi ya muda wote, familia yangu, programu za vijana, na baadhi ya waumini wenye mahitaji makubwa. Hakukuwa na muda wa kutosha kumtembelea kila muumini mara kwa mara.

Hata hivyo, kama askofu, Roho wakati mwingine alinipa msukumo kumtembelea muumini fulani ambaye alikuwa akisumbuka. Mara nyingi, matembezi hayo yalianza kwa wao kusema “Nilijua ungekuja.” Mara nyingi tulimhisi Roho kwa wingi pale wote tulipotambua kwamba kutembelea kule kulikuwa ni uthibitisho kwamba Mungu hujibu sala.

Na pia mara zote nilifurahia mapokezi niliyoyapata mlangoni kwa wale wenye kushiriki kikamilifu, waumini “wasio na matatizo.” Watu hawa wazuri huenda kanisani kila wiki, hutumikia kiuaminifu katika miito, hawana changamoto kubwa, na mara nyingi hawapati matembezi toka kwa viongozi wa ukuhani. Walikuwa na shukrani kuwa na wakati wa uso kwa uso na askofu wao. Kwenu nyote ninasema, “Asante! Endeleeni! Jueni kwamba askofu wenu anawapenda na angependa kuwatembelea zaidi kama angeweza.”

7. Askofu wenu kiukweli, hasa, kwa uaminifu anawahitaji mhudumiane.

man on the phone

Kama askofu, kila mara nilipoambiwa muumini wa kata ambaye alikuwa akitatizwa, mara zote ningeuliza, “akina nani ni walimu wa nyumbani na waalimu watembeleaji?” Hii ilikuwa njia moja wapo ya kutathmini kwamba mahitaji ya waumini yangetimizwa vyote kwa muda mrefu na mfupi. Askofu, akifanya kazi bila msaada toka kwa waumini wa kata au kigingi, ana rasilimali zenye ukomo. Ni hakika kwamba anaweza—na ataweza—kwenda kuwatembelea watu katika matatizo. Lakini kwa rasilimali za ukuhani na Muungano wa Usaidizi wa akina Mama zinazopatikana kwake, ufikiaji wake unaweza kuwa mkubwa.

Hivi ndivyo kuhudumia kunavyokuwa. Kuna nyakati ambapo baadhi yetu tunasahau kwa nini tunahudumiana: Bwana alituamuru sisi “Kupendana” (Yohana 13:34). Jueni kwamba askofu wenu hutumia uhudumiaji kama njia ya muongozo wa kiungu ya “kuwepo zaidi” katika maisha ya waumini wa kata.

8. Askofu anatamani angefanya kila awezalo kwa ajili ya kundi lake.

man walking up

Muda wowote, mchana au usiku, iwe ni baraka ya ukuhani, ushauri kwa mtoto aliyepotea njia, au kuwahi katika eneo la ajali, angependa kufanya chochote muumini angehitaji. Hawezi mara zote kuyafanya yote, na anaweza asiwe mtu mahususi katika kila hali, lakini usiogope kumuomba msaada wakati unapouhitaji. Jua kwamba askofu yuko kwa ajili ya kuhudumia katika nyakati hizo na kwamba nyote mnabarikiwa sana kwa kufanya kazi pamoja.

Ninanyenyekezwa kwa fursa tukufu niliyokuwa nayo ya kuhudumia katika wito huu mtakatifu. Katika huduma yangu, nilikwenda kutoka kwenye kuamini mpaka kwenye uelewa. Sina shaka tena kwamba injili ni ya kweli; ninajua ni ya kweli. Sina shaka tena kwamba Mungu ananijua; ninajua kwamba Mungu anatujua bila mwisho kila mmoja wetu, maisha yetu ya kila siku na masumbuko yetu binafsi. Zaidi, ninajua kwamba Anafanya kazi kupitia watumishi Wake, hasa wale wanaoshikilia funguo za ukuhani. Ninajua kwamba nisingeweza kuhudumia kama askofu bila usilivu wa Mungu kwa ajili ya kazi hii. Ni ukweli wa injili na upendo wa Mungu kwa watoto Wake ambao unamwezesha kila askofu kuhudumia.

Muhtasari

  1. Thomas S. Monson, “Wajibu wa Miito,” Ensign, Mei 1996, 44.