Njia5 za Kujifunza Kutoka kwenye Mkutano Mkuu
Mkutano mkuu ni fursa ya ajabu ya kuungana na waumini wa Kanisa ulimwenguni kote kusikiliza viongozi wa Kanisa na kupokea maelekezo kutoka kwa Bwana. Kuangalia, kusikiliza, na kusoma hotuba za mkutano mkuu kutamleta Roho katika maisha yako na kusaidia kujenga ushuhuda wako. Ni fursa kwako kupokea na kufanyia kazi ufunuo binafsi.
Hapa kuna njia tano ambazo unaweza kujifunza kutoka kwenye mkutano mkuu.
1. Andika maswali yako kabla ya mkutano mkuu kuanza
Chukua muda kuandika maswali yako kabla ya mkutano mkuu kuanza, na kisha kuwa makini kwa majibu ambayo yanakuja kwako wakati wa mkutano mkuu. Sala na maswali yako yanaweza kujibiwa unaposhiriki na kumsikiliza Roho.
2. Tafuta kujifunza kuhusu Kristo
Manabii wanashuhudia na kufundisha kuhusu Mwokozi (ona Matendo ya Mitume 10: 43). Unaposikiliza hotuba za mkutano mkuu, ungeweza kufikiria kuhusu nini mzungumzaji anakufundisha kuhusu Yesu Kristo. Ungeweza hata kuweka orodha ya muhtasari wako.
3. Tafuta dhamira
Baada ya kutazama baadhi ya mkutano mkuu, ungeweza kugundua kwamba umesikia mada au dhamira zilizotajwa zaidi ya mara moja. Mipangilio uliyoigundua inaweza kuwa ni njia mojawapo Roho anakusaidia wewe kutambua kitu fulani unachohitaji kujifunza.
4. Zingatia Kitabu cha Mormoni
Unaweza kujifunza mambo mengi kwa kuwa makini na maandiko ambayo viongozi wa kanisa wanayarejea hasa Kitabu cha Mormoni, ambacho ni “jiwe kuu la tao la dini yetu” (utangulizi wa Kitabu cha Mormoni). Jaribu kuona kama unaweza kuweka kumbukumbu ya kila mara kinapotajwa kwenye mkutano mkuu. Utastaajabishwa na utakachopata!
5. Kuwa mwenye ari na mwenye msukumo kutenda
Andika hotuba na nukuu ambazo zinakutia msukumo wa kiungu au zinazokualika kutenda. Hii inaweza kukusaidia kutumia yale unayojifunza—na kukusaidia kukumbuka mawazo yako yalikuwa ni yapi baadae wakati ukihitaji ukumbusho!