Jinsi Gani Bwana Amekuwa Mwenye Rehema
Toleo jipya la majuzuu la historia ya Kanisa litatusaidia sisi kutunza maagano yetu kwa kupanua kumbukumbu zetu juu ya kile Mwokozi ametutendea.
Kwa mara ya kwanza karibu miaka mia moja, toleo jipya la majuzuu ya historia ya Kanisa linachapishwa chini ya ulelekezi wa Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Likiwa na kichwa cha Watakatifu: Hadithi ya Kanisa la Yesu Kristo katika Siku za Mwisho, hii historia simulizi inaelezea hadithi ya kweli ya watu wa kawaida ambao walikuja kuwa Watakatifu kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo (ona Mosia 3:19). Toleo la kwanza The Standard of Truth, 1815–1846, sasa limekamilika na limetafsiriwa katika lugha 14 kwa ajili ya kusambazwa maeneo mengi ulimwenguni.
Watakatifu ni hadithi ya jinsi Mungu alivyorejesha agano Lake lisilo na mwisho kwa sababu ya Upendo Wake kwa watoto Wake. Huonyesha jinsi gani Bwana alivyorejesha injili Yake ili kutoa tumaini na amani katika nyakati za ghasia, majaribu, na masumbuko. Huoyesha pia jinsi gani maagano yaliyorejeshwa huongoza katika kuinuliwa kupitia Yesu Kristo.
Ungeweza kutegemea hadithi kuanza na Joseph Smith, lakini Watakatifu huanzia mnamo 1815 kwa mlipuko wa volcano huko Indonesia, ambao ulisababisha vifo kwa wingi, ugonjwa na usumbufu. Dondoo ya mwanzo huu ilichaguliwa katika kile ambacho Bwana alikifunua kuhusu jinsi gani Alirejesha maagano ambayo yanatuunganisha sisi na Mwokozi na kutuwezesha kushinda matatizo yote ya maisha.
“Mimi Bwana, nikijua majanga yajayo juu ya wakazi wa dunia, nimemwita mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, na kusema naye kutoka mbinguni, na nikampa yeye amri; …
“Kwamba agano langu lisilo na mwisho liweze kuanzishwa” (M&M 1:17, 22).
Kutoka tukio la ufunguzi wake mpaka usambazwaji wake ulimwenguni kote, Watakatifu huashiria kwa watoto wote wa Mungu kila sehemu kwamba ni hadithi ya agano lao na Mungu, ambaye anayajua magumu yao. Kupitia nabii Wake, Mungu alifanya upya maagano ambayo hayaondoi uovu, huzuni, masumbuko, na utengano wakati wa kifo lakini yanayoahidi uponyaji kupitia Upatanisho wa Mwokozi, utakaso na kuzawadia maisha yetu kwa maana isiyoelezeka, na kutuhakikishia kwamba mahusiano tunayoyafurahia hapa duniani yanaweza kudumu milele, “yakizidishwa na uzima wa milele” (ona M&M 130:2).
Sura nane za kwanza za The Standard of Truth zimechapishwa katika matoleo ya jarida hili kwa mwaka mzima. Toleo la mwezi huu linahitimisha sura zilizofanywa kwa msururu toka kwenye Watakatifu, lakini hadithi inaendelea katika saints.lds.org, kwenye Gospel Library App, na kwa nakala iliyochapishwa (agiza kupitia store.lds.org). Ninawaalika muendelee kuisoma katika sehemu yoyote ya njia hizi.
Mfumo na Mpango Mtukufu
Watakatifu huendeleza mfumo mtakatifu ambao manabii, kama sehemu yao ya huduma, hutumia yaliyopita kutusaidia kujifunza sisi ni kina nani na kuona makusudi ya Mungu katika maisha yetu. Katika maandiko, manabii wengi wanaanza mafundisho yao kwa kurejea katika hadithi za rehema ya Bwana kwa mababu zao.1 Moroni aliwaomba kwa dhati wasomaji wa Kitabu cha Mormoni “kukumbuka jinsi vile Bwana amekuwa na huruma” katika historia yote na “kutafakari katika mioyo yenu” (Moroni 10:3). Kutafakari kuhusu ukarimu wa Mungu hutuandaa sisi kupokea ushahidi wa Roho, ambao hutufundisha “kuhusu vitu vilivyo kiuhalisia kwa sasa, na kiuhalisia vitakavyokuwa” (Yakobo 4:13; ona pia Moroni 10:4–5).
Kujua kwamba Wazazi Wetu wa Mbinguni walipanga hatima ya furaha yetu na kuinuliwa hutupatia kusudi, hutupatia utambulisho kama watoto wapendwa wa wazazi waliotukuka, na huongeza ujasiri wetu katika Bwana, hata katika nyakati za majaribu. Kukumbuka ukarimu wa Bwana kunaweza pia kutukinga dhidi ya kiburi na majanga ya ukwasi. Mormoni aliandika kuhusu wakati ambapo Wanefi “walianza kuwa matajiri sana.” Lakini tofauti na nyakati zingine kwenye Kitabu cha Mormoni ambapo watu waliruhusu kiburi na utajiri kuleta kuanguka kwao, walifuata njia nyingine wakati huu “Lakini ijapokuwa utajiri wao, au nguvu yao, au mafanikio yao, hawakujiinua kwa kiburi machoni mwao; wala hawakuwa wavivu wa kumkumbuka Bwana Mungu wao; lakini walijinyenyekeza sana mbele yake.” Walishika maagano na kubakia watakatifu kwa sababu “walikumbuka ni vitu gani vikuu Bwana alikuwa amewatendea wao” (ona Alma 62:48–50).
Watakatifu hufundisha masomo kama haya na mengine mengi. Itakusaidia kuona mkono wa Bwana katika maisha yako wakati unapopata uzoefu kwa niaba wa majaribu ya imani, kuvunjika moyo na shangwe, ufunuo na urekebishwaji wa watu wasio wakamilifu waliompenda Bwana na waliohisi upendo Wake.
Wakati unasoma, utagundua umaizi mpya na maana hata katika hadithi ambazo umewahi kuzisikia awali. Hakuna tukio katika historia ya Kanisa linalojulikana zaidi kuliko Ono la Kwanza la Joseph Smith, lakini Watakatifu hutusaidia kuelewa vizuri zaidi jinsi gani Joseph alihangaika kuleta katika usawa kile alichohisi katika moyo wake na kile alichofikiri kwenye mawazo yake.
Nia ya dhati ya Joseph kuhisi msamaha wa Mwokozi ilikwenda bila kutimia kwa sababu aligundua kwamba hakuna kanisa kati ya yale yaliyokuwepo lilifundisha “injili ya Yesu Kristo kama ilivyoandikwa kwenye Agano Jipya.”2 Katika mawazo yake Joseph alitafakari ni kanisa lipi lilikuwa sahihi au kama yote yalikuwa si sahihi. Moyoni mwake kwa kukata tamaa alitumaini kwamba moja kati ya hayo lilikuwa sahihi ili aweze kupata amani aliyoitafuta. Kichwani mwake na moyoni mwake akiwa hajui nini cha kufanya, Joseph aligundua kwamba angeweza kumuuliza Mungu. Alikwenda kijisituni kusali. Huko alimwona Baba na Mwana, ambao walimsamehe na kutatua sintofahamu yake katika njia ambayo hakuwahi kuifikiria.3
Joseph, familia yake na watu wengine wengi ambao walishikilia maagano ya Bwana yaliyorejeshwa walitaka kuhisi upendo wa Mungu kwao, kujifunza namna gani wangeweza kusogea karibu Naye, na kuponya uhusiano pamoja na wapendwa. Watakatifu husimulia hadithi zao.
Kumwamini Bwana Katika Nyakati za Majaribu
Juzuu namba 1 la Watakatifu linajumuisha hadithi ya kuumiza moyo ya Amanda Barnes Smith na familia yake, ambao walitii amri za Bwana na walikuwa wakitenda mapenzi Yake.4 Mume wa Amanda na mmoja wa wana wake waliuawa kikatili pamoja na Watakatifu wa Siku za Mwisho wengine 15 waliokuwa wamepiga kambi katika sehemu ndogo ya makazi karibu na kijito cha Shoal huko Missouri. Bwana alimshikilia Amanda katika uzeofu huu mbaya, akijibu sala zake, akimtia moyo, na kumwezesha kumponya mwana wake aliyejeruhiwa vibaya.5
Watakatifu huonyesha jinsi gani Amanda alijifunza kumtegemea Bwana katika dhiki kali sana. Pia huongelea kuhusu kile Joseph Smith alijifunza kuhusu Upendo wa Mungu hata katika nyakati za mateso. Huonyesha kwamba kwa kujua matendo ya Bwana hutupatia kusudi la milele, hutusaidia kuona vitu kiuhalisia kama vilivyo na kiuhalisia vitakavyokuwa, na hutusaidia kutumia imani kwamba Bwana atatuvusha katika nyakati ngumu.
Wakati nabii Joseph Smith alijua kilichotokea kwenye familia ya Amanda na wengine katika kijito cha Shoal, alihisi ingekuwa bora angeenda jela au kuuliwa kuliko kuwaacha Watakatifu kuuwawa. Siku iliyofuata alijaribu kuweka maridhiano ya amani na jeshi la mgambo la Missouri, ambalo lilikuwa likijulikana kwa kushambulia makazi makuu ya Watakatifu ya Far West. Badala yake Joseph alikamatwa na kushikiliwa kama mfungwa.
Karibu miezi mitano baadae, Joseph alibakia chini ya ulinzi, akiwa kwenye baridi, kwenye gereza la chini lenye nafasi ndogo huko Liberty, Missouri Alijiuliza Mungu alikuwa amejificha wapi na ni kwa muda gani Angesimama kusikiliza vilio vya wajane na yatima. Alisali, “Ee Bwana, ni kwa muda gani watateseka kwa maovu haya na dhuluma zisizo za kisheria, kabla moyo wako haujalainika kwa ajili yao, na matumbo yako kusikia huruma kwa ajili yao?” (M&M 121:3).
Watakatifu hutufundisha kwamba jaribu si uthibitisho wa Bwana kutotupenda, au kujitoa kwa baraka Zake. Upinzani ni sehemu ya mpango wa Mungu kututengeneza sisi na kutuandaa kwa ajili kudra ya Selestia, ya milele (ona 2 Nefi 2:11). Joseph Smith alijifunza kwamba mateso ya Bwana yasiyo na mwisho Humwezesha kutusaidia sisi wakati tunapoteseka na hatimaye kutuinua (ona Alma 7:11–13). Kwa kujibu kilio cha uchungu cha Joseph, Bwana aliorodhesha aina zote za chanagamoto kabla hajahitimisha:
“Kama mataya yale ya jahanamu yataachama kinywa wazi kwa ajili yako, fahamu wewe, mwanangu, kwamba mambo haya yote yatakupa wewe uzoefu, na yatakuwa kwa faida yako.
“Mwana wa Mtu ameshuka chini yao wote. Je, wewe u mkuu kuliko yeye?” (M&M 122:7–8).
Kwa sisi wenyewe kupata uzoefu wa vitu hivi kunaweza kutuzawadia huruma ya Kristo kwa ajili ya wale wanaoteseka. “Moyo wangu mara zote utakuwa wenye huruma zaidi baada ya hili kuliko vile ungeweza kuwa hapo awali,” Joseph alitambua akiwa gerezani. Alitamani angeweza kuwa pamoja na Watakatifu kuwafariji na kuwatia moyo. “Kamwe sikuweza kuhisi kama ninavyohisi sasa,” alielezea, “Kama nisingetendwa uovu niliyoteseka.”6
Sababu moja ya Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kuruhusu na kutoa idhini ya toleo la Watakatifu ni kwamba linaweza kumsaidia kila mmoja wetu kupata uzoefu wa vitu hivi kupitia hadithi za wengine. Tunaweza kujifunza kutoka kwa Amanda kwamba hata wakati Mungu anaona sawa katika hekima Yake kutozuia uovu au mateso, anatupenda na Anatujali. Anasikia sala zetu na ni mwenye rehema na fadhili.
Urejesho wa Baraka za Hekaluni
Hakuna sehemu yoyote ambapo rehema hii na fadhili huonyeshwa kwa wingi zaidi ya Hekaluni. Katika kiini chake Watakatifu ni hadithi ya urejesho wa baraka za hekaluni. Juzuu la kwanza linamalizika wakati maelfu ya Watakatifu wa Siku za Mwisho wakipokea ibada takatifu katika hekalu la Nauvoo mwaka 1846. Juzuu la pili litafikia kilele cha uwekaji wakfu wa hekalu la Salt Lake na Watakatifu wakianza kupokea ibada humo mwaka 1839. Juzuu la tatu litahitimisha kwa Watakatifu toka bara la Ulaya wakianza kukusanyika kwenye hekalu huko Switzerland mwaka 1955. Juzuu la nne litatoa hadithi mpaka wakati huu wa sasa, wakati mahekalu yakijaza dunia na Watakatifu kote ulimwenguni wakipokea ibada za kuinuliwa, kama manabii walivyoona hapo zamani.
Katika nyumba ya Bwana tunaweka maagano na tunapokea zawadi ya nguvu za kushinda matokeo ya Anguko, ikijumuisha uovu na mateso katika dunia hii. Tunapokea ulinzi na hatimaye nguvu za Kufufuka, tukiwa tumeunganishwa na wapendwa milele.
Toleo la Watakatifu litatusaidia kushika maagano kwa kupanua kumbukumbu zetu katika njia za sakramenti. Litatusaidia mara zote kukumbuka kile mwokozi ametutendea. Bila kumbukumbu ya matendo ya Mungu katika nyakati za kale, tusingeweza “kukumbuka jinsi vile Bwana amekuwa na huruma kwa watoto wa watu” (Moroni 10:3). Kwa sababu hizi, tuna deni kwa Bwana na kwa Watakatifu ambao waliweka kumbukumbu za uzoefu wao wa upendo Wake kwao. Bwana alimwamuru Joseph Smith kuweka kumbukumbu ya uzoefu wake (ona M&M 121:1). Alimwamuru mwana historia wa Kanisa akiwa chini ya uelekezi wa Joseph Smith “Kuweka kumbukumbu za kanisa bila kukoma” (M&M 47:3). Aliamuru kwamba historia ijumuishe “vitu vyote ambavyo ni vizuri kwa kanisa, na kwa vizazi vinavyochipukia” (M&M 69:8).
Kwa mafunuo haya na ahadi ya agano ya daima kumkumbuka Mwokozi akilini, Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili walianza kupanga toleo la Watakatifu miaka 10 iliyopita. Sasa tunawahimiza kulisoma, tukiamini litawasaidia katika kuelewa mpango wa Mungu, kuona ni kwa jinsi gani Bwana amekuwa mwenye rehema, mkivumilia kwa uaminifu katika nyakati nzuri na mbaya, mkipata huruma ya Kristo kwa ajili ya wengine, na mkishika maagano yawaongozayo katika kuinuliwa.