“Je, Misheni na Huduma ya Kristo Ilikuwa ni Nini?,” Liahona, Jan. 2023.
Njoo, Unifuate
Je, Misheni na Huduma ya Kristo Ilikuwa ni Nini?
Yesu Kristo alifanya agano kwenye maisha ya kabla ya haya la kuja Duniani na kuwa Mwokozi wetu (ona Musa 4:2; Ibrahim 3:27). Kama Mwokozi wetu, Yeye alikamilisha vyote misheni na huduma Yake.
Rais Russell M. Nelson alieleza: “Misheni ya Bwana hapa duniani ilikuwa ni kukamilisha Upatanisho … [na] kufanya uzima wa milele uwezekane kwa kila mtu ambaye ataustahili. … Huduma Yake ilikuwa kila kitu chochote ambacho alifanya—miujiza Yake, mafundisho Yake, upendo Wake, fokasi Yake kwenye ibada takatifu, mafundisho Yake kwetu ya jinsi ya kusali.”1
Vipengele vya misheni na huduma ya Kristo vimeelezwa kwenye sehemu nyingi katika maandiko. Angalia maelezo yaliyotolewa na mama yake, Mariamu, katika Luka 1:46–55. Hana, pia ni mfano wa unyenyekevu, alitoa sala kama hiyo kuhusu huduma ya Bwana katika 1 Samweli 2:1–10.
Kama kitabu cha kiada cha Njoo,Unifuate kinavyopendekeza, unaweza kulinganisha haya na Mahubiri ya Mlimani katika Mathayo 5:3–12.2
Fikiria kuorodhesha baadhi ya vipengele vya huduma ya Kristo ambavyo maandiko haya yanavielezea; kipengele kimoja kimeorodheshwa kama mfano:
-
Kristo alikuja kusaidia kushibisha njaa yetu ya kiroho (ona 1 Samweli 2:5; Luka 1:53; Mathayo 5:6).