“Jinsi Gani Tumebarikiwa na Nuru ya Ulimwengu?,” Liahona, Jan, 2023.
Njoo, Unifuate
Jinsi Gani Tumebarikiwa na Nuru ya Ulimwengu”?
Yohana alikuja “kuishuhudia ile Nuru,” “Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu” (Yohana 1:7, 9). “Nuru itokayo kutoka uwepo wa Mungu … [na] “inatoa uhai kwa vitu vyote”(Mafundisho na maagano 88:12–13).
Jinsi gani nuru inatubariki sisi? Ona Alma 19:6,; 36:20; Mafundisho na Maagano 88:67.
Nuru imehusishwa na nini? Ona Mafundisho na Maagano 84:45.
Jinsi gani tunakua katika nuru? Ona Mafundisho na Maagano 93:28.
Nani ni Nuru ya Ulimwengu? Ona Yohana 8:12; 3 Nefi 18:16, 24.
Rais Lorenzo Snow (1814–1901) alifundisha, “tunaamini kwamba roho ambayo inaiangaza familia ya mwanadamu inakuja kutoka uwepo wa Mwenyezi, kwamba inasambaa kila mahala, kwamba ni nuru na uhai wa vitu vyote, na kwamba kila moyo mnyoofu unakuwa nayo kwa uwiano wa wema wake, uadilifu na tamaa yake ya kujua ukweli na kufanya mema kwa wanadamu wenzake”.(Mafundisho ya Lorenzo Snow, ed. Clyde J. Williams [1996], 107).