“Ujumbe Wangu kutoka kwa Bwana,” Liahona, Jan. 2024.
Taswira za Imani
Ujumbe Wangu kutoka kwa Bwana
Nilijifunza kwamba kufundisha kutoka katika Kitabu cha Mormoni ilikuwa ni njia nzuri ya kupata ushuhuda wangu juu ya kitabu hiki.
Mnamo 1993, siku tatu baada ya kuhamia Polokwane, kaskazini mwa Afika ya Kusini, nilisikia mlango wa nyumba ukigongwa. Wakati nilipofungua, mlangoni walisimama wamisionari wawili wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.
Nililelewa katika mazingira ya dini, na familia yangu daima wamenionya kukaa mbali na wamisionari. Lakini walionekana kuwa wazuri na nilifurahia kuzungumza nao kuhusu dini, hivyo niliwakaribisha waingie ndani.
Baada ya maongezi mazuri, waliniambia,“Je, tunaweza kukupa Kitabu cha Mormoni?”
“Subirini, subirini kidogo,” nilijibu. “Nafikiri ninacho kimoja.”
Nilipowaonyesha nakala yangu, walishangazwa. Niliwaeleza kwamba katika mji wa nyumbani kwetu Cape Town, miaka mingi iliyopita, wamisionari walinipa Kitabu cha Mormoni kwenye maonyesho. Nilikitunza, na kila baada ya muda nilifunua kurasa zake.
Baada ya maongezi yetu, niliwakaribisha wamisionari kurudi tena. Nimelelewa katika kanisa tofauti, ambako, baba yangu wa kambo alikuwa mtumishi huko. Wazo la kubatizwa tena likawa moja ya vikwazo vya uongofu wangu. Licha ya hayo, nilianza kuhudhuria tawi dogo la Kanisa hilo. Baada ya mwaka mmoja na nusu hivi, rais wa tawi aliniita ofisini mwake.
“Tunataka Wewe Upate Ushuhuda”
“David, ninataka nikupe changamoto,” rais wa tawi alisema. “Hakika tunataka wewe upate ushuhuda juu ya Kitabu cha Mormoni. Ninahisi unaweza kufanya hilo kama nitakuita wewe ufundishe Mafundisho ya Injili. Tayari wewe unafundisha kule Chuo Kikuu, na huogopi kusimama mbele za watu.”
Leo, walimu lazima wawe waumini wa Kanisa.1 Lakini huko nyuma, rais wa tawi alihisi kupata mwongozo wa kuniomba mimi kufundisha. Ninashukuru kwa hilo.
“SAWA,” nilisema.
Kila Jumamosi usiku ningejifunza somo kwa kirefu ili niweze kulielewa, kulijua na kulihusisha na hadithi na tabia za Kitabu cha Mormoni Kwangu mimi, hakika ilikuwa njia nzuri ya kupata ushuhuda wake.
Jumapili moja, baada ya kuwa nimefundisha kwa karibia mwaka mmoja, rais wa misheni kutoka Pretoria alikuja kwa ajili ya mkutano na akahudhuria darasa langu la Shule ya Jumapili.
“Asante, Kaka Baxter,” alisema baadaye. “Hilo lilikuwa somo zuri. Wewe unatoka wapi?”
Nilipomwambia natoka Cape Town, aliniuliza ni kata gani nimekuwa nikihudhuria.
“Sikuwa nimehudhuria kata.”
“Unamaanisha nini?” aliuliza.
“Mimi ni yule ambaye ungemtaja kama Myunani?” Nilisema. “Mimi si muumini wa Kanisa.”
Alibadilika sura na kuwa nyeupe usoni na akaharakisha kwenda kwa rais wa tawi.
“Unaye mtu asiye muumini wa Kanisa anafundisha maandiko?” rais wa misheni alimuuliza rais wa tawi.
“Ndio, je, amefundisha vibaya?”
“Hapana.”
“Je, alikuwa anafundisha kwa mwongozo wa kiungu?”
“Ndiyo”
“Je, alifundisha mafundisho ya Kweli?
“Ndiyo.”
Wakanirusu kuendelea kufundisha. Miezi michache baadaye, nilienda kuitembelea familia yangu kule Cape Town kwa ajili ya sikukuu za Krismasi. Nilipokuwa huko, mama yangu akaniambia alikuwa anakwenda kuliacha kanisa lake baada ya baba yangu wa kambo kufariki. Katika muda huo huo, Bwana akaniachilia huru dhidi ya hisia yoyote ya hatia niliyokuwa nayo kwa sababu ya utiifu wangu kwa mama yangu na kanisa nililokulia.
Niliporudi nyumbani, nilimwita yule rais wa tawi.
“Ningependa nibatizwe kesho,” nilimwambia.
“David una uhakika?”
“Hakika,” nilisema. “Nimepata ujumbe kutoka kwa Bwana.”
“Nina Kitu cha Kukupa”
Nilipomwambia Baba yangu mzazi kwamba nimekuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, sikuelewa kwa nini amekuwa mkimya sana.
“Acha nikueleze kidogo juu ya historia yangu.
Baba yangu ambaye kamwe hajawahi kuzungumza na mimi kuhusu dini, alinieleza kwamba kama mvulana, amekuwa akihudhuria Kata ya Kumora ya Kanisa huko Cape Town. Ameichezea timu ya kata hiyo ya mpira wa kikapu. Alitengeneza marafiki kadhaa wa karibu ambao walikuwa Watakatifu wa Siku za mwisho. Mmoja wa marafiki wake wakubwa alikuwa mmisionari ambaye, baada ya misheni yake, aliuawa huko Vietnam.
Kama baba yangu asingempoteza rafiki huyo, nadhani angekuwa amejiunga na Kanisa. Maisha yake yangekuwa ni hadithi moja tofauti na sasa. Miaka mingi baadaye, bado anayo heshima kubwa sana kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho. Hakuwahi kujiunga na dini yoyote, lakini hakika aliunga mkono uamuzi wangu wa kujiunga na Kanisa.
Miezi michache baada ya baba yangu wa kambo kufariki nilimwambia mama yangu kuhusu ubatizo wangu. Hilo nalo halikupita vyema pia. Hata hivyo, nilipoenda huko Uholanzi kutembelea familia ya Kidachi wanafamilia upande wa mama yangu, nilishiriki uongofu wangu pamoja nao. Hapo ndipo nilipojifunza juu ya familia nyingine tunayoungana nayo kwenye Kanisa.
Wakati wa matembezi yangu, mjomba alinijia. “Nina kitu maalumu ninataka kukupa,” mjoma alisema. Alinipa nakala ya toleo la kwanza la Kitabu cha Mormoni kwa Kidachi, kilichochapishwa mwaka 1890.
“Kimekuwa mali ya familia yetu kwa miaka mingi,” alisema. “Ninataka uwe nacho wewe.”
Muunganiko huu wa familia mbili Kanisani ulikuwa faraja kwangu mimi sana. Leo, ninakienzi kile Kitabu cha Mormoni kwa Kidachi. Kinanikumbusha juu ya wale wamisionari wa kwanza walionitembelea. Kinanikumbusha juu ya jinsi gani kufundisha Kitabu cha Mormoni kulivyokuwa muhimu kwa uongofu wangu. Kinanikumbusha juu ya heshima ya marehemu baba yangu kwa Kanisa na kwamba baadhi ya mababu zangu wameipokea injili ya urejesho.
Pia inanikumbusha kwamba Kitabu cha Mormoni hakika kina nguvu ya kuwashawishi wote “Myahudi na Myunani kwamba Yesu ndiye Kristo, Mungu wa Milele, akijidhihirisha mwenyewe kwa mataifa yote.”2