Liahona
Bogotá, Colombia
Januari 2024


“Bogota, Colombia,” Liahona, Jan. 2024.

Kanisa Liko Hapa

Bogotá, Colombia

ramani ikiwa na duara kuzunguka Colombia
mandhari ya mtaani huko Bogotá, Colombia

Bogota ni mojawapo ya miji mikuu iliyo uwanda wa juu sana ulimwenguni. Tawi la kwanza la Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho katika Colombia liliundwa mnamo 1966. Leo, Kanisa huko Colombia lina:

  • Waumini 214,400 (kwa makadirio)

  • Vigingi 30, kata na matawi 257, misheni 5

  • Mahekalu 2 (Bogota na Barranquilla) na 1 limetangazwa (Cali)

Nyimbo za Dini humwalika Roho.

Dario na Esneda Cruz, kutoka Bogotá, wanahisi kuwa karibu zaidi na Mungu wanapoimba nyimbo za dini. “Kupitia nyimbo tunaimarisha shuhuda zetu”, wanaelezea. “Hisia zinazoleta kwenye mioyo yetu ni kitu maalumu.”

Waumini wa Kanisa wanaimba kutoka kwenye kitabu cha nyimbo za dini nyumbani.

Zaidi kuhusu Kanisa huko Colombia

  • Rais Dallin H. Oaks, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, na Mzee Ulisses Soares wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili wanasafiri kwenda Colombia kwa ajili ya kuweka wakfu hekalu huko Barranquilla.

  • Waumini huko Colombia hukuza kujitegemea na matumaini, licha ya mapambano.

  • Soma jinsi gani mshiriki wa Sabini kutoka Colombia alivyojiunga na Kanisa.

  • Rais Oaks anashiriki hadithi ya wanandoa waaminifu huko Colombia na dhabihu waliyofanya ili kuunganishwa hekaluni.

  • Kigingi huko Colombia kinatoa muda na kufanya kazi ili kuisaidia familia yenye shida.

Hekalu la Barranquilla Colombia

Hekalu la Barranquilla Colombia

Waumini wakisimama kwa ajili ya kupiga picha nje ya hekalu

Waumini wakiwa wanapiga picha nje ya Hekalu la Barranquilla Colombia kabla ya kuwekwa wakfu mnamo Desemba 2018.

Rais Dallin H. Oaks na wengine kwenye uwekaji wakfu wa hekalu

Rais Dallin H. Oaks, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza wa Kanisa, aliweka wakfu Hekalu la Barranquilla Colombia mnamo Desemba 9, 2018.

kwaya kwenye uwekaji wakfu hekalu

Waumini wanakusanyika kuimba katika kwaya kwa ajili ya uwekaji wakfu hekalu.

Rais Dallin H. Oaks akisalimiana kwa kushikana mikono na mvulana

Wakati wa ziara yake huko Barranquilla, Rais Oaks alisalimiana kwa kushikana mikono na mvulana kwenye ibada fupi ya vijana.