Liahona
Toleo Letu Bora Zaidi
Januari 2024


“Toleo Letu Bora Zaidi,” Liahona, Jan. 2024.

Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Toleo Letu Bora Zaidi

Tunapoweka wakfu hekalu, Tunasema kwa Bwana, “Hili hapa ni toleo letu. Ni zuri kadiri tulivyoweza kulifanya.”

Viwanja vya hekalu

Takribani wiki mbili kabla ya kuweka wakfu upya Hekalu la Washington D.C mnamo Agosti 2022, mimi pamoja na mkuu wangu wa kazi tuligundua kwamba moja ya miti ya European hornbeam katika njia ya kuelekea hekaluni ulionekana kuwa na ugonjwa. Ulikuwa umepungua katikati na ulikuwa na mikwaruzo kwenye matawi yake.

Kama mtunza bustani za hekalu, nilitatizika kwamba viwanja vya hekalu zuri vilikuwa tayari isipokuwa kwa sehemu hii ndogo. Mti ulikuwa pembeni na chemichemi irukayo juu jirani na mlango wa hekalu.

Tulikuwa na mti wa kuchukua nafasi yake wenye afya uliokua ukiota karibu yake, na tulijadili uwezekano wa kuweka ule mti wenye afya na kuondoa ule uliokuwa na ugonjwa. Lakini kwanza tungepaswa kuondoa njia ya waenda kwa miguu iliyo jirani na nyasi na kisha kuhamisha kinyunyizia maji na waya za umeme zinazopita katika eneo hilo. Hofu yangu kubwa ilikuwa kwamba tungeutoa mti ule wenye ugonjwa, kuoanda ule wenye afya, na kukosa muda wa kutosha kufanya kila kitu kuzunguka ule mti paonekane vizuri kwa ajili ya kuweka wakfu upya.

Nilipomwambia mke wangu, Carolyn, kwamba yawezekana tukauondoa ule mti, alisema: “We yapunguze yale matawi yenye mikwaruzo, na mimi nitawaomba akina dada wenzangu wa maandiko nchi nzima tusali kwa ajili ya mti huo. Viwanja vya hekalu ni vya Bwana. Yeye ataubariki mti huu.”.

Carolyn ana kikundi cha marafiki anaowaita akina dada wa maandiko—waumini wa Kanisa ambao walikuwa wakiishi katika kata moja. Walijifunza Njoo, Unifuate kwa pamoja hadi wote walipohama, lakini bado wanawasiliana. Sala inapohitajika, wanaitana.

Baada ya Carolyn kuwaambia kuhusu mti wenye ugonjwa, wao waliwaambia watoto wao na wanafamilia wengine. Carolyn hakujua ni watu wangapi walioomba kwa ajili ya mti ule, lakini alikuwa na imani kwamba Baba wa Mbinguni angesikia sala zao.

Ndani ya siku chache, mti ule ulichipua majani mapya, yakajaza lile eneo lenye uchache wa majani. “Ndiyo, unaonekana mzuri zaidi,” Carolyn alisema. Akatuma picha za mti kwa wale akina dada wa maandiko, akiwaambia, “Tazameni jinsi gani Bwana alivyotujibu!”

Nilijua kwamba watu walikuwa wakiuombea mti, hivyo wala sikushangaa. Pia nilijua kwamba Rais Russell M. Nelson hivi punde angelibariki hekalu na viwanja vya hekalu wakati wa sala ya kuweka wakfu. Mti utakuwa SAWA.

Tulishukuru kwamba Bwana alikuwa ameheshimu toleo na imani yetu.