Liahona
Je, Mimi ni “Mzamiaji” au “Mpiga Mbizi”?
Januari 2024


“Je, Mimi ni ‘Mzamiaji’ au ‘Mpiga Mbizi’?,” Liahona, Jan. 2024.

Njoo, Unifuate

1 Nefi 6–10

Je, Mimi ni “Mzamiaji” au “Mpiga Mbizi”?

Mtu anazama ndani ya maji

Katika ndoto ya Lehi ya mti wa uzima (ona 1 Nefi 8), kwa nini unafikiri baadhi ya watu waliuacha mti wakati wengine walibaki kwenye mti ili kula lile tunda? Baadhi ya watu waliokula tunda walianguka, waliona aibu kwa kuzomewa na umati mkubwa uliokuwa katika jengo kubwa na pana. Tofauti moja kubwa kati ya yale makundi inatokana na kile walichokifanya kabla hawajafika pale: jinsi gani walishikilia ile fimbo ya chuma—neno la Mungu.

Kung’ang’ania au Kushikilia kwa Nguvu

Lehi aliwaona wale waliokuwa “wakisonga mbele … waking’ang’ania kwenye fimbo ya chuma” na wale ambao “walikuwa wakisonga mbele, daima wameshikilia kwa nguvu kwenye fimbo ya chuma” (1 Nefi 8:24, 30; msisitizo umeongezwa).

Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili amesema kwamba yale makundi matatu yalianza safari pamoja, lakini ni makundi mawili tu walishikilia kwenye fimbo ya chuma:

“[Kundi la pili] pia walipata baraka ya ziada ya fimbo ya chuma, na walikuwa wameing’ang’ania! … Kung’ang’ania fimbo ya chuma kunapendekeza kwangu ujifunzaji wa hapa na pale wa ‘ghafla’ au kuzama kusikofuata kanuni badala ya kupiga mbizi kuliko endelevu katika neno la Mungu. …

“Kundi la tatu pia lilisonga mbele kwa imani na kusadiki; hata hivyo, hakuna ishara kwamba walizurura mbali. … Labda kundi hili la tatu la watu kwa uaminifu walisoma na walijifunza na walipekua maandiko. … Hili ndilo kundi ambalo wewe na mimi tunapaswa tujitahidi kujiunga nalo.”1

Je, sisi ni “wazamiaji” au “wapiga mbizi” inapokuja kupata uzoefu wa neno la Mungu? Ingawa wote wazamiaji na wapiga mbizi hulowa, wapiga mbizi wanao uzoefu wa kina na endelevu zaidi ambao unaweza kuleta furaha endelevu.