“Kuwa Shahidi,” Liahona, Jan. 2024.
Njoo, Unifuate
Kurasa za Utangulizi za Kitabu cha Mormoni
Kuwa Shahidi
Mnamo majira ya kuchipua ya mwaka 1829, Mary na Peter Whitmer walimkaribisha Joseph na Emma Smith na Oliver Cowdery nyumbani mwao ili tafsiri ya mabamba ya dhahabu iweze kukamilika. Mahitaji ya muda wa Mary yalikuwa juu sana. Aliwahudumia watu tisa katika nyumba yake mwenyewe na kuwasidia watoto wake waliooa walioishi jirani na yeye.
Wana watano wa Mary na vijana wa kiume wote wawili ambao (hatimaye) walikuja kuwa wakweze walikuja kuwa mashahidi rasmi wa yale mabamba ya dhahabu mnamo Juni 1829. Mwezi ule ule, Mary alipokea ushahidi huo yeye mwenyewe.
Nje ya nyumba yake, mwanaume mwenye mvi akiwa na gunia kwenye bega lake alimjia Mary na kusema, “Jina langu ni Moroni. Umekuwa mwenye uchovu mwingi kwa sababu ya kazi za ziada unazozifanya.” Akishusha gunia lile kutoka begani mwake, Moroni aliendelea, “Wewe umekuwa mwaminifu sana na mwenye bidii katika kazi zako. Ni sahihi, kwa hiyo, kwamba unapaswa kupokea ushahidi ili imani yako ipate kuimarika.” Ndipo kisha akafunua yaliyokuwemo katika gunia lake—yale mabamba ya dhahabu.1
Mary akawa shahidi wa yale mabamba ya dhahabu, kama wale Mashahidi Watatu na mashahidi Wanane ambao shuhuda zao ziko katika kurasa za utangulizi za Kitabu cha Mormoni. Unyenyekevu wa Mary na juhudi vilimwandaa kuwa shahidi. Ushuhuda wake haujaandikwa katika kurasa za utangulizi za Kitabu cha Mormoni, na jina lake haliko juu ya mabango, makumbusho au katika akili za Watakatifu wengi waliofuatia baada yake. Ingawa mchango wake wa kila siku katika nyumba yake na familia yake umepita pasipo kutambulika na wengi, walijulikana na Mungu.
Mzee Dieter F. Uchtdorf wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha:
“Bwana anahukumu tofauti sana na njia ambazo sisi tunahukumu. Yeye anapendezwa na watumishi watukufu, siyo wenye kujitukuza wenyewe.
“Wale walio wanyenyekevu katika maisha haya watavikwa mataji ya utukufu katika maisha yajayo.”2
Kumbukumbu ya Moroni sasa imetafsiriwa katika Kitabu cha Mormoni, na tunaweza kupata ushahidi wa ukweli wake kulingana na ahadi Moroni aliyoiacha katika kurasa zake za mwisho. “Ningewasihi kwamba mungemwomba Mungu, Baba wa Milele, katika jina la Kristo, kama vitu hivi sio vya kweli, na kama mtamwomba kwa dhati, na nia moja, mkiwa na imani katika Kristo, atawaonyesha ukweli wake kwa uwezo wa Roho Mtakatifu” (Moroni 10:4).
Je, umewahi kuhisi kama mzigo wako ni mkubwa lakini jitihada zako zinapita bila kutambulika? Baba wa MbingunI anakujua wewe, na anajua mema unayofanya. Kadiri unavyoenda ukifanya mema (ona Matendo 10:38), ukihudumu bila kupiga makelele, na ukiyapekua maandiko, Roho Mtakatifu anaweza akatibitisha ukweli wa injili kwako.
Watoto wa Mary na Peter Whitmer
Christian Whitmer |
Jacob Whitmer |
John Whitmer |
David Whitmer |
Catherine Whitmer (Page) |
Peter Whitmer |
Elizabeth Ann Whitmer (Cowdery) |
Mmoja wa Mashahidi Wanane |
Mmoja wa Mashahidi Wanane |
Mmoja wa Mashahidi Wanane |
Mmoja wa Mashahidi Wanane |
Aliolewa na Hiram Page, mmoja wa Mashahidi Wanane |
Mmoja wa Mashahidi Wanane |
Aliolewa na Oliver Cowdery, mmoja wa Mashahidi Watatu |