“Yesu Kristo katika Kitabu cha Mormoni,” Liahona, Jan. 2024.
Yesu Kristo katika Kitabu cha Mormoni
Ni mara ngapi Yesu Kristo anatajwa katika Kitabu cha Mormoni?
Ni nani ungesema ndiye mtu mkuu katika Kitabu cha Mormoni? Wakati watu wengine wangependekeza kuwa ni Nefi, Alma au Mormoni , kwa kweli mtu mkuu ni Yesu Kristo. Nefi aliandika:
“Tunafanya kazi kwa bidii kuandika, ili kuwashawishi watoto wetu … kuamini katika Kristo. …
“Na tunazungumza juu ya Kristo, tunashangilia katika Kristo, tunahubiri juu ya Kristo, tunatoa unabii juu ya Kristo” (2 Nefi 25:23, 26).
Mnamo 1978, Susan Ward Easton alichapisha makala maarufu, katika tarakimu inaonyesha kwamba Yesu Kristo ni mtu mkuu katika Kitabu cha Mormoni. Yeye alionyesha majina tofauti ya Yesu Kristo na kuonyesha kwamba alikuwa ametajwa kwa jina au cheo mara 3,925 katika Kitabu cha Mormoni ambacho kwa wastani kila baada ya mistari 1.7.1
Somo hili la thamani linaweka alama ya ukuu wa Mwokozi katika Kitabu cha Mormoni; hata hivyo, kwa kipekee somo hili linatoa idadi chache kwa kutozingatia viwakilishi ambavyo vinatumika kumtaja Kristo.
Mwishowe, idadi ya marejeo kwa Yesu Kristo siyo maelezo muhimu ya kujifunza katika Kitabu cha Mormoni, ingawa, kila rejeo kwake Yeye linaweza kutufundisha sisi kuhusu asili yake ya kiungu na misheni Yake. Kwa uangalifu tunachunguza Kitabu cha Mormoni, tukitazama kutajwa kote kwa Yesu Kristo, ikijumuisha vyeo na viwakilishi. Tumeona jumla ya marejeo 7,452—wastani wa zaidi ya rejeo moja kwa kila mstari.2 Vyeo vya Kristo vinachukua kwa wastani wa asilimia 50 ya marejeo ya Kristo katika Kitabu cha Mormoni, na yanayobakia yanakuja kutoka katika viwakilishi.
Kumtazama Yesu Kristo kunatoa njia ya kipekee ya kujifunza kuhusu Yeye. Zingatia jinsi gani mstari unaofuata unavyomsisitiza Yeye: “Anza kuamini katika Mwana wa Mungu, kwamba Yeye atakuja kukomboa watu wake, na kwamba yeye atateseka na kufa ili kulipia dhambi zao; na kwamba yeye atafufuka tena kutoka kwa wafu, ambao utaleta ufufuko, kwamba watu wote watasimama mbele yake,wahukumiwe katika siku ya mwisho na ya hukumu, kulingana na matendo yao” (Alma 33:22; mkazo umeongezwa).
Katika mafunzo ya awali ya Dada Easton, mstari huu ungelihesabika kama rejeo moja la Kristo kutoka jina la “Mwana wa Mungu.” Hata hivyo, Mwokozi ametajwa mara tano zaidi. Mstari huu hausisitizi tu kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu bali pia kwamba Yeye ndiye mwenye kutukomboa sisi kupitia Upatanisho Wake usio na mwisho na Ufufuko na atakuwa mwamuzi Wetu.
Pengine kwa uwezo mkubwa zaidi, Kristo anajirejelea Yeye mwenyewe katika Kitabu cha Mormoni. Kwa mfano, tunasoma Mwokozi akisema, “Kama watu watakuja kwangu mimi nitawaonyesha madhaifu yao. Mimi natoa kwa wanadamu udhaifu ili wapate kuwa wanyenyekevu; na neema yangu inatosha kwa wanadamu wote kwamba wajinyenyekeshe wenyewe mbele yangu; kwani kama watajinyenyekeza wenyewe mbele yangu, na kuwa na imani katika mimi, kisha mimi nitafanya vitu dhaifu kuwa imara kwao” (Ether 12:27; msisitizo umeongezwa). Ingawa jina la Kristo halionekani katika mstari huu, Mwokozi anarejelea kwake Yeye mwenyewe mara nane. Nafasi Yake imesisitizwa tunapomtafuta Mwokozi katika kifungu hiki cha maneno.
Mistari ifuatayo inaonyesha muunganiko wa kibinafsi ambao Mwokozi aliuhisi kwa kila mtu binafsi na kile watu walikihisi Kwake Yeye.
“Inukeni na mje kwangu, ili msukume mikono yenu kwenye ubavu wangu, na pia kwamba mguse alama za misumari katika mikono yangu na katika miguu yangu , ili mjue kwamba Mimi ni Mungu wa Israeli, na ni Mungu wa ulimwengu wote, na nimeuawa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu.
“… Na ikawa kwamba umati ulienda mbele, na kusukuma mikono yao ubavuni mwake na wakaona alama za misumari katika mikono yake na katika miguu yake ” (3 Nefi 11:14–15; msisitizo umeongezwa).
Ingawa hatuwezi kiuhalisia kuhisi alama Zake kupitia Kitabu cha Mormoni tunaweza kuongeza ushahidi wetu binafsi juu ya Yesu Kristo.
Marejeo ya mara kwa mara kwa Bwana katika Kitabu cha Mormoni hutusaidia sisi kuona ukuu Wake katika kazi hii takatifu. Kumtambua Yesu Kristo katika Kitabu cha Mormoni: Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo ni njia yenye nguvu ya kujongea karibu zaidi na Yeye.