“Je, Ni Kitu Gani Kinafanya Maandiko kuwa ‘ya Thamani Kuu’?,” Liahona, Jan. 2024.
Njoo, Unifuate
Je, ni Kitu Gani Kinafanya Maandiko Kuwa “ya Thamani Kuu”?
Maandiko yalikuwa “ya thamani kuu” (1 Nefi 5:21) kwa familia ya Lehi. Yalikuwa muhimu sana kiasi kwamba Bwana aliamuru watoto wa Lehi wasafiri kurudi hadi Yerusalemu ili kuchukua mabamba ya shaba (ona 1 Nefi 3:2–5), kazi ambayo ilihatarisha maisha yao. Maandiko (hususani Kitabu cha Mormoni) vile vile ni muhimu kwetu sisi leo. Je, umewahi kufikiria hivi karibuni kuhusu kwa nini ni muhimu?
Je, ni kitu gani mabamba ya shaba yaliipa familia ya Lehi? |
Je, Kitabu cha Mormoni kinatupa nini sisi leo? |
Maneno ya manabii (1 Nefi 3:20) |
Msingi wa ushuhuda wa Joseph Smith, Urejesho, na manabii walio hai (Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni) |
Hadithi ya Uumbaji na Adamu na Hawa (1 Nefi 5:11) |
Mafundisho ya ufafanuzi kuhusu mpango wa wokovu (2 Nefi 2; Alma 12; 34) |
Sheria ya Musa (1 Nehi 4:15–16) na amri nyinginezo (1 Nefi 5:21) |
Mafundisho ya Kristo na amri nyinginezo (2 Nefi 31; 3 Nefi 11; 27) |
Kumbukumbu ya Wayahudi na ushahidi wao juu ya Kristo (1 Nefi 5:12) |
Mashahidi wa ziada wa Kristo kutoka “kondoo Wake wengine” (3 Nefi 15:21–24) |
Kumbukumbu ambayo ilihifadhi lugha ya baba zao (1 Nefi 3:19) na koo zao (1 Nefi 5:14) |
Kumbukumbu ambayo inaweza kutusaidia sisi kuwakusanya Israeli waliotawanyika (3 Nefi 21:6–7) |