Liahona
Kupanda Upya Mbegu ya Imani
Machi 2024


“Kupanda Upya Mbegu ya Imani,” Liahona, Machi 2024.

Kupanda Upya Mbegu ya Imani

Masomo kutoka kwa wale waliorudi kwenye imani

mashina ya miti na matawi

Katika ulimwengu ambao mara nyingi unakuza hadithi za kupotea kwa imani, safari za kimya kimya za wanaorudi kwenye imani wakati mwingine hazipati kutambulika. Lakini hadithi za kuongoka tena zinaonesha jinsi akina kaka na akina dada katika injili wanavyoshinda wasiwasi wao hata baada ya kuliacha Kanisa. Hadithi zao zinaonesha kile Alma anachofundisha kuhusu kupanda mbegu. Alma anaeleza mchakato wa imani ambao unasaidia kuwaimarisha wale wanaojaribu kukuza imani yao lakini pia unawasaidia wale wanaopambana na maswali na mashaka.

  • “Kwanza, tunahitaji kuelewa kwamba “imani siyo kuwa na uelewa kamili” (Alma 32:21).

  • Kisha “tunatumia chembe ya imani “ au hata “hamu tu ya kuamini” (mstari wa 27).

  • Tunapanda mbegu—neno la Mungu—katika moyo wetu (ona mstari wa 28).

  • Njiani, tunarutubisha mizizi yetu ya kiroho kwa subira na kukubali msaada kutoka kwa marafiki katika injili ili kuukuza mti uliopandwa katika Kristo, “utakaokua hata kwenye uzima wa milele” (mstari wa 41).

“Imani siyo kuwa na ufahamu kamili wa vitu; kwa hivyo mkiwa na imani, mnatumainia vitu ambavyo havionekani, ambavyo ni vya kweli”.(Alma 32:21).

Alba Fonseca

Alba Lucia Fonseca, muumini wa Kanisa kutoka Marekani, aliona kifaa mtandaoni ambacho kiliibua wasiwasi kuhusu imani yake ya kidini, na alipitia upotevu wa haraka wa imani. Kwanza, alitupa mbegu ya imani kwa mashaka yake, lakini kisha alianza kuzungumza na muumini anayejali na mwenye ufahamu na alitambua kwamba kutoamini kwake pia kuliibua maswali.

“Uelewa wangu wa dhana za injili na wa historia ya Kanisa haukuwa mpana kama nilivyodhani,” yeye anaeleza. “Hiyo ilinifanya niwe mnyenyekevu na ilinisaidia nielewe kwamba bado nilikuwa na mengi ya kujifunza na kwamba imani haiji kwa maswali yote kujibiwa.” Alba alitambua kwamba vitu vingine vya maana katika maisha—kama vile familia, elimu, kazi—vinahusisha hatari, dhabihu, mashaka, na juhudi ya maisha yote. Nilirudi Kanisani na ninaweza kuthibitisha kwamba kudumisha imani pia kunastahili aina hii ya juhudi.

Rais Russell M. Nelson alifundisha “Bwana hahitaji imani kamili kwetu ili tufikie uwezo Wake mkamilifu”. Na bado imani yetu, anabainisha, inahitaji juhudi endelevu ili iendelee kukua.1 Wakati msingi wa mwanzo wa Hekalu la Salt Lake ulipohimili vizuri kwa zaidi ya karne, sasa unahitaji ukarabati mkubwa, Rais Nelson alieleza. Sisi pia lazima wakati mwingine tuimarishe misingi yetu ya kiroho “ili kushinda hatari kubwa zijazo na mashinikizo.”2 Wakati mwingine tunapokabiliana na mambo magumu kama Alba aliyokabiliana nayo, tamanio letu kwa ajili ya uhakika linaweza kutuongoza kutoka kwenye imani ya kawaida kwenda kwenye kutokuamini, tukiacha juhudi muhimu za kuimarisha na kuuongezea nguvu msingi wetu wa kiroho.

Wale wanaojifunza hadithi za wanaorudi kwenye imani wamegundua zinawasaidia kuiangalia imani kama safari ya maisha yote, yenye hatua nyingi.3 Tungeweza kuanza na imani ya kawaida kama mtoto, lakini mahali fulani imani ile ya kitoto inakabiliwa na maswali na wasiwasi. Wakati imani yetu isiyojaribiwa inaweza kuwa imetuhudumia vyema kama msingi wa kiroho, lazima sasa twende mbele kutoka kwenye imani ya kawaida kupitia ugumu hadi imani iliyokomaa ambayo inaweza kuhimili changamoto zijazo.4 Kuacha imani inaweza kuonekana rahisi sana, takribani kama faraja, lakini utajiri wenye thawabu unafuatana na safari za wale wanaomgeukia Mungu na kuendelea kurutubisha mbegu zao za imani.

Majaribu ya imani yalianza kwa Samuel Hoglund wa Sweden wakati wanafamilia walipozua maswali. Alipitia hatua ya “kupata kujibiwa swali moja tu na kuona swali jingine bado linahitaji kujibiwa,” anaeleza. “Imani yangu iliyumbayumba kutoka nusu saa moja kwenda inayofuata, mpaka nilipotambua kwamba mchakato huu na mahitaji yangu kwa ajili ya uhakika vilikuwa haviwezi kukidhi mahitaji hayo.” Badala ya kujaribu kukusudia kutatua kila swali dogo, Samuel aliamua kujifunza maswali muhimu—yale yaliyo muhimu kwa msingi imara katika Yesu Kristo. Ikifuatiwa na sala na kujifunza maandiko, utafutaji wa Samuel, kama vile wa Alba, ulimfundisha ni kiasi gani bado anahitaji kujifunza na ulimleta kwenye imani zilizokomaa zaidi. “Uzoefu huu uliimarisha imani yangu kwa kiasi kikubwa,” alisema, “na pia ulinifundisha kwamba kile unachokitafuta kweli utakipata.”

“Ikiwa mtaamka na kuziwasha akili zenu, hata kwenye kufanyia majaribio juu ya maneno yangu na kutumia chembe ya imani, ndiyo, hata ikiwa hamwezi ila kutamani kuamini, acha hamu hii ifanye kazi ndani yenu” (Alma 32:27).

“Kuonesha imani kunaweza kuonekana ya kuchosha,” Rais Nelson alikubali. “Wakati mwingine tunaweza kujiuliza kama tunaweza kupata imani ya kutosha kupokea baraka ambazo tunazihitaji sana.”5 Lakini hata hatua ndogo za imani, zikianza na “chembe ya imani,” zinaweza “kufanya kazi ndani yako” na kuanza uzaliwaji upya kiroho.

Baada ya kuzurura kiroho katika miaka yake ya chuoni, Amanda Freebairn wa Marekani alichukua hatua ndogo ya kusali, ambayo ilimwongoza kufuata ushawishi wa kutembelea viwanja vya hekalu la eneo lake. “Kumhisi Roho pale kuliamsha tena imani yangu,” anasema. Kurudi Kanisani na kukubali wito wa kufundisha Msingi kuliongeza imani yake, na aliendelea kuchukua hatua ambazo zilimpeleka kwenye kukumbatia injili kikamilifu. Njiani, Amanda anasema, “nilipata majibu ya maswali niliyojiuliza sana.”

Dan Ellsworth

Wakati mmoja, Dan Ellsworth, pia kutoka Marekani hakuwa na uhakika ya kuwa alikuwa na chembe ya imani iliyobaki kuionesha. Hatua zake za mwanzo kwenye elimu na kutumia mbinu za kihistoria kuelewa Agano la Kale vilidhoofisha imani yake katika Biblia na kuathiri kuamini kwake katika maandiko yote. Lakini Dan aliendelea kwenda Kanisani na aliamua kufanyia majaribio mpango wa kusali, kufunga, na kuhudumia Kanisani kwa miezi sita. Wakati mwingine, alimwomba pia binti yake mdogo kusali kwa ajili ya imani ya baba.

Baada ya muda, Dan alianza kuwa na uzoefu wa kiroho na kupata majibu kwa baadhi ya maswali ambayo yalimsumbua sana. Siku moja, akiwa kwenye maktaba, alihisi kushawishiwa kwenda chini ya safu ya vitabu na kuchagua kimoja. Ndani yake, alipata utambuzi ulio kinyume na hoja za kwenye kitabu ambacho hapo mwanzo kilitikisa imani yake katika Biblia. Wakati uzoefu huu haukujibu kila swali, ulimfundisha Dan baadhi ya masomo muhimu: “Kwanza, nilihitaji kuwa mnyenyekevu kuhusu kiasi gani ningeweza kujua mimi mwenyewe. Na pili, njia zingine za kutafuta ukweli, pamoja na sababu, zipo: misukumo ya kiroho, matokeo chanya kutokana na tunda la Roho, na mawazo ambayo yanakimu uvumbuzi wa kiakili, yote ambayo yaliongoza kwenye kusadiki kwa nguvu sana na imani kuliko ile ambayo nilikuwa nayo kabla.”

Zac Marshall na familia

Kwa Zac Marshall kutoka Uingereza, hatua ya kawaida ya kuangalia video za kielimu kuhusu Kitabu cha Mormoni zilifungua akili yake kwa uwezekano kwamba kitabu kinaweza kuwa chenye kukubalika. “Nilishakisoma hapo mwanzo katika kujifunza maandiko kama familia na mimi mwenyewe binafsi pasipo kusudi halisi,” anaeleza. “Lakini nijiondoa kuwa mwenye kushiriki kikamilifu Kanisani kama kijana, kwa hiyo ushahidi niliouona katika video ulinisababisha nikisome Kitabu cha Mormoni kwa kusudi kwa mara ya kwanza.” Baada ya kufanyia majaribio neno la Mungu, Zac alianza kubadilisha wasiwasi kwa imani. Sasa anasema, “Kanisa nililoliona wakati mmoja kama lenye kuzuia sasa naliona kama lenye kukomboa katika njia ile ile Yesu anayosema, ‘Ukweli utakuweka huru’ [Yohana 8:32].”

“Lakini mkiuachilia mti ule, na msifikirie kuulisha, tazama hautapata mzizi wowote” (Alma:32:38).

Wakati tukichukua hatua ndogo ndogo kurutubisha imani, pia tunahitaji kuwa na ufahamu wa njia zetu za kufikiri ambazo zinapinga na kuzuia imani. Katika kujifunza hadithi za kurudi-kwenye imani za waumini wa Kanisa katika nchi mbalimbali, Eric na Sarah d’Evegnée, maprofesa kwenye Chuo kikuu cha Brigham Young–Idaho, wameona kwamba “Jinsi tunavyofikiri inaweza kuwa muhimu kama kile tunachofikiri.” Kwa mfano, kutegemea kwamba kujitolea kidini kutatulinda na usumbufu na changamoto za maisha zenye kuumiza moyo siyo kweli na kunajenga mawazo yasiyo halisi. Yesu Kristo aliahidi kutotuacha kamwe, lakini alitahadharisha kwamba “Ulimwenguni mnayo dhiki” (Yohana 16:33). Bado, changamoto za maisha zinaweza, kulingana na Sarah, “kutuongoza kuiona injili kwa njia hasi. Wakati mwingine tunatupa nje maadili wakati tunapokabiliana na chochote kilicho chini ya maadili.”

Mtunzi na mwana historia wa jujitegemea Don Bradley wa Marekani alikutana na maswali kuhusu historia ya Kanisa wakati ambapo, anaeleza, “sikuwa tu na furaha na nilikuwa nashuku matarajio. Ubeuzi kuhusu yeyote unaweza kwa njia hasi kuathiri uhusiano, na nilipoteza imani na uhusiano wangu na Mungu.” Miaka mingi baadaye, Don alianza kufanya kazi kuelekea tumaini na shukrani katika maisha yake binafsi.

Pia alianza kutafiti masomo kuhusu faida za afya ya akili na mwili za dini yenye mpangilio. “Sikuweza kukataa masomo hayo,” Don anakumbuka. “Taratibu, nilitambua nilikuwa nimebadilisha kushuku kuwa fikra zenye tija na mtazamo wenye tumaini zaidi kwenye maisha, niliipata tena imani yangu katika Mungu na Yesu Kristo.” Don alirudi kwenye taarifa ya kihistoria ambayo mwanzo aliIng’ang’ania, lakini sasa nyenzo hii ileile ilimwongoza kwenye kumsadikisha kwamba Joseph Smith alikuwa nabii wa Mungu.

“Kama mtalirutubisha neno, ndio, kurutubisha mti unapoanza kukua, … ndio utavuna thawabu ya imani yako, na bidii yako, na uvumilivu, na subira” (Alma 32:41, 43).

Hata kwa utayari wa kufanyia mazoezi neno la Mungu na kuwa na akili iliyotulia ya tumaini, kurudi kwenye imani na kwenye mahudhurio Kanisani kunaweza kukatisha tamaa, takribani mchakato wenye kuchosha. Juhudi zinahitaji si tu uvumilivu, ujasiri, na unyenyekevu lakini pia upendo wa marafiki na wanafamilia. Kukubali msaada wa marafiki wa kweli kunarutubisha mbegu na kuiruhusu itoe mizizi badala ya kunyauka.

Leo Winegar

Wakati Leo Winegar wa Marekani kwa mara ya kwanza alipokabiliana na maswali kuhusu historia ya Kanisa, alijifunza umuhimu wa marafiki wenye huruma. “Ushuhuda wangu ulinyauka,” anaeleza, pale alipopitia kipindi cha “upweke na giza la kukata tamaa kabisa wakati nilipopambana kusali.” Siku moja Leo alihisi kushawishiwa kuwasiliana na profesa wa historia ya Kanisa. Siyo tu alimtia moyo Leo kufikiria upya njia yake ya wasiwasi bali pia alikuwa rafiki wa karibu. Ushuhuda wa Leo pole pole ulirudi kwa msaada wa mnasihi wake na miaka ya matumaini ya kujifunza. Baada ya muda, alipata majibu kwa maswali yake mengi. “Ninahisi shukrani milele kwa Mwokozi wangu Yesu Kristo kwa kuniongoza kurudi,” anaeleza, “na kwa marafiki ambao walimwakilisha Yeye.”

“Kama marafiki na familia … wanaacha Kanisa, endelea kuwapenda,” alishauri Rais Nelson. “Si juu yako kuhukumu uchaguzi wa mwingine zaidi ya wewe unavyostahili kukosolewa kwa kubakia mwaminifu.”6

Letitia Rule

Woga wa ukosoaji kama huo ulimweka Letitia Rule, muunimi wa Uingereza, mbali na injili kwa miaka 20. Mara nyingi alitaka kurudi, lakini “alikuwa mwoga wa kutembea tu kupitia mlangoni, akihisi kuhukumiwa na kama vile sikuwahi kuishi kwa usahihi.” Ni uchunguzi uliotishia maisha tu ndiyo ulimpa ujasiri wa kuchukua hatua ile ngumu. Waumini walimkaribisha kwa ukarimu na upendo, wakimsaidia atake kushiriki katika injili tena.

“Pandeni neno hili kwenye mioyo yenu, na litakapoanza kuvimba endeleeni kulilisha kwa imani yenu. Na tazama, litakuwa mti, ukikua ndani yako kwenye maisha yasiyo na mwisho” (Alma 33:23).

Alma anapomaliza mahubiri yake, anaweka wazi kwamba wakati juhudi za kurutubisha mbegu ni muhimu sana, juhudi siyo mbegu yenyewe. Badala yake, tunapanda mbegu ya kweli wakati “tunapoanza kuamini katika Mwana wa Mungu, kwamba atakuja kuwakomboa watu wake, na kwamba atateseka na kufa ili alipie dhambi zao” (Alma 33:22).

Michael Auras kutoka Ujerumani alijifunza masomo muhimu kuhusu vipaumbele vya injili baada ya kuasi kama kijana. “Mambo mengi mno mazuri na uhusiano mzuri vipo hai katika injili, lakini ni imani tu katika Yesu Kristo itahimili shuhuda zetu,” anaeleza. “Mimi na baba yangu wote tulisita katika imani yetu kwa muda kwa maswali mbalimbali lakini tulirudi wakati tulipoweka msingi wa imani yetu katika Yesu Kristo zaidi ya kila kitu kingine chochote.”

Rais Nelson anatuhakikishia, “Mwokozi daima yupo karibu sana na wewe wakati unapokabiliana na milima au kupanda mlima kwa imani.”7 Yesu Mwenyewe anaahidi, “Mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari” (Mathayo 28:20). Atatembea pamoja nasi, atatupenda “kwa upendo usio na mwisho” (Yeremia 31:3), na kutupatia uzima tele (ona Yohana 10:10). Wale walio radhi kupanda mbegu hii wataona kwamba hata imani yao ndogo inaweza, kupitia Mwokozi, kuwa “mti utakaokua ndani yako kwenye maisha yasiyo na mwisho” (Alma 33:23).

Mwandishi anaishi Utah, Marekani.

Muhtasari

  1. Ona Russell M. Nelson, “Kristo Amefufuka; Imani Kwake Itahamisha Milima,” Liahona, Mei 2021, 102-3.

  2. Russell M. Nelson, “Hekalu na Msingi Wako wa Kiroho,” Liahona,, Nov. 2021, 93.

  3. Ona Bruce C. Hafeh na Marie K Hafen, Imani siyo Upofu ( 2018).

  4. Imani yetu katika [Yesu Kristo] inaweza na itatuongoza kupita magumu ya maisha. Kwa hakika, tutagundua kwamba kuna urahisi kwenye upande mwingine wa magumu tunapobaki ‘[thabiti] katika Kristo’ [2 Nefi 31:20]” (Larry S Kacker, “Ngazi ya Imani,” Liahona, Mei 2022, 25)

  5. Russell M. Nelson, “Kristo Amefufuka;,” 102.

  6. Russell M. Nelson, “Choices for Eternity” (worldwide devotional for young adults, May 15, 2022), broadcasts.ChurchofJesusChrist.org.

  7. Russell M. Nelson, “Kristo Amefufuka;,” 103.