“Ninawezaje Kujumuisha Kitabu cha Mormoni katika Desturi Zangu za Pasaka?,” Liahona, Machi 2024.
Njoo, Unifuate
Pasaka
Ninawezaje Kujumuisha Kitabu cha Mormoni katika Desturi Zangu za Pasaka?
Kitabu cha Mormoni kinatoa ushahidi wenye nguvu juu ya ukweli wa Bwana aliyefufuka, Yesu Kristo. “Sisi kama Watakatifu wa Siku za mwisho tumepewa zawadi kubwa mno ya Pasaka … kitabu cha Mormoni.”1
Rais Russell M. Nelson alifundisha, “Sababu kubwa ya sisi kusherehekea Krismasi ni kwa sababu ya Pasaka.”2 Kwa namna sawa na jinsi baadhi ya familia wanavyosoma au kuigiza hadithi ya Krismasi kutoka Luka 2 wakati wa Krismasi, familia yako ingeweza kutumia shughuli zinazoambatana na kumsherehekea Mwokozi aliyefufuka katika Pasaka hii kwa kutumia 3 Nefi 11:1–17. Nyimbo zilizoorodheshwa zinahusiana na mistari iliyochaguliwa, lakini ungeweza pia kuchagua nyimbo zako za dini unazozipenda kuhusu Yesu Kristo.
Shughuli
Ukiwa na wanafamilia au wewe mwenyewe, soma na uimbe kuhusu Yesu Kristo akija kwa Wanefi baada ya Kufufuka Kwake.
Soma |
Sikiliza au Imba |
“This Is My Beloved Son,” mstari wa 2, Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 76. | |
“Did Jesus Really Live Again?,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 64. | |
“Easter Hosanna,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 68–69 |