Liahona
Unastahili Kuwa wa Mahala Hapa
Machi 2024


“Unastahili Kuwa wa Mahala Hapa,” Liahona, Machi 2024.

Vijana Wakubwa

Wewe ni wa Hapa

Tunaweza kupata hisia yetu ya kustahili kuwa wa mahala fulani tunapojenga uhusiano na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Mungu Baba na Yesu Kristo wakiinyoosha mikono yao katika kuwasalimu watu wanaowazunguka.

Maelezo kutoka Utukufu katika Madaraja, na Annie Henrie Nader

Kila mmoja wetu alizaliwa na asili ya kuhitaji kustahili kuwa wa mahala fulani. Kwa asili tunatamani sana kustahili kuwa wa mahala fulani katika michangamano yetu na familia, marafiki, wafanyakazi wenzetu, kata, na watu wengine katika maisha yetu. Mioyo yetu inaonekana kuwa na matamanio haya ya mbinguni kwa ajili ya mahitaji ya kina na ya kudumu ya kustahili kuwa wa mahala fulani.

Wewe na mimi tulikuwa—na bado ni—sehemu ya familia ya milele pamoja na Baba wa Mbinguni, muda mrefu kabla hatujaja duniani. Maandiko yanatuelezea sisi kama “wageni na wasafiri hapa duniani” (Waebrania 11:13; Mafundisho na Maagano 45:13). Katika kuondoka nyumbani kwetu mbinguni na kuja kwenye ulimwengu uliojaa vurugu, upweke, na huzuni kubwa, tunaweza kuhisi kama wazururaji, tukitamani kurudi kwenye nyumba yetu na uhusiano wetu wa milele.

Kama umewahi kuhisi kidogo kutamani nyumbani mbinguni, pengine ni kwa sababu nyumba yetu ya kweli na utambulisho wetu wa kweli vimeunganishwa kwa Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi, Yesu Kristo. Hiyo ndiyo sababu ya kwa nini ni muhimu sana kuwa na muunganiko wa kina pamoja Nao. Tunapokuwa tumeunganika Nao kupitia uhusiano wetu wa agano, tutapata hisia ya kweli ya kustahili kuwa wa mahala fulani ambayo nafsi zetu zinaitamani sana.

Uhusiano Wetu wa agano na Mungu

Matendo yetu na mawazo yetu yanaonesha mahusiano tunayoyathamini. Hilo pia ni kweli juu ya uhusiano wetu wa agano na Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi.

Tunapothamini agano letu la uhusianio na Mungu, kila kitu hubadilika. Badala ya kushawishiwa na ulimwengu, ttunashawishiwa na Yeye na kuwa zaidi kama Yeye. Maisha yetu yanaanza kuwa na uthabiti zaidi na utulivu wa kiroho na nguvu. Ghafla, “kustahili kuwa wa mahala fulani” kunapita fahari za maisha ya duniani ya kile tunachodhani “kustahili kuwa wa mahala fulani” humaanisha.

Wakati uhusiano ule wa agano na Mungu unapokuja kwanza, vivuta mawazo vitupu vya ulimwengu vinapoteza mashiko yake na tunapata amani binafsi ya kweli na kustahili kuwa wa mahala fulani. Katika ulimwengu ambao mara nyingi hautoi vitu bila malipo, Baba yetu wa Mbinguni kwa upendo ananyoosha baraka za agano Lake bila kujali hadhi zetu katika ulimwengu huu (ona 2 Nefi 9:50–51).

Rais Russell M. Nelson kwa uzuri alifundisha kwamba “mara tunapofanya agano na Mungu, tunaacha uwanda wa katikati milele. Mungu hatatupilia mbali uhusiano Wake na wale ambao wameunda mfungamano kama huo na Yeye. Kwa hakika, wale wote ambao wamefanya agano na Mungu wana njia ya kupata aina maalumu ya upendo na rehema.”1

Tunaamua kama tuna uhusiano wa karibu na Mungu—Yeye siku zote habadiliki kwetu, lakini ni lazima tuchague kutobadilika Kwake. Na uchaguzi huo mtakatifu unawezesha na kuweka huru! Uchaguzi huu unatuweka huru kutokana mitizamo ya uongo ya sisi ni akina nani na kutokana na minyororo yenye kikomo ya matarajio ya kiulimwengu.

Na wakati tutakapopata kustahili huko kuwa wa Baba yetu wa Mbinguni, tunaweza kisha kuangalia upande wa nje na kuwaona wengine kama Yeye anavyowaona. Ninapoelewa jinsi Yeye anavyohisi kunihusu mimi, naelewa vyema jinsi anavyohisi kuwahusu nyinyi, na uwezo wangu na hamu yangu ya kunyoosha mkono na kuwakusanya wengine inakuwa thabiti sana.

Hekalu la Nauvoo wakati wa machweo ya jua.

Kielelezo cha Hekalu la Nauvoo wakati wa machweo ya jua, na Max D. Weaver

Maagano Hufungua Baraka

Baba yetu wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatamani sisi tufanye Nao maagano ili Waweze kutubariki katika njia tunazohitaji na kutubadilisha katika njia ambazo zitaturuhusu kurudi kwenye uwepo Wao.

Ningekualika wewe kwenda mara nyingi uwezavyo kwenye nyumba ya Bwana. Ninapoweka sharti la kwenda mara kwa mara na kwa madhumuni, ninapokea nafuu kutokana na mambo ya ulimwenguni, na mawazo yangu na asili yangu vinainuliwa.

Kupitia kushika maagano yetu, tunapokea nguvu ya ukuhani ambayo inafungua baraka za Upatanisho wa Mwokozi katika maisha yetu. Baraka hizo zinajumuisha uponyaji, mwongozo, ulinzi, msaada, uimara, amani, mtazamo, na furaha. Baba wa Mbinguni anatamani kutubariki kwa vitu vyote hivi kupitia uhusiano wetu wa agano.

Kama bado hujapokea baraka za hekaluni, ninakualika ujifunze baraka za hekaluni, nguvu ya ukuhani, maagano, na kile ambacho Mungu anatamani kwa ajili yako. Usikawie kupokea faraja Yake, nguvu, na, msaada wa upendo.

Rais Nelson amesema:

“Ninakusihi sana usingoje mpaka ufunge ndoa ndipo upate endaumenti ndani ya nyumba ya Bwana. Anza kujifunza sasa na kupata uzoefu wa kile inachomaanisha kujihami kwa nguvu ya ukuhani.

“Na kwa kila mmoja wenu ambaye amefanya maagano ya hekaluni, ninawasihi mtafute—kwa sala na kwa uendelevu—kuelewa maagano na ibada za hekaluni. Milango ya kiroho itafunguka. Utajifunza jinsi ya kufungua pazia kati ya mbingu na dunia, jinsi ya kuomba malaika wa Mungu wakuhudumie na namna nzuri ya kupokea mwongozo kutoka mbinguni. Juhudi zako za bidii za kufanya hayo zitaimarisha na kutia nguvu msingi wako wa kiroho. “2

Kustahili kuwa wa mahala fulani kupitia Toba

Toba ya mara kwa mara ni njia nyingine yenye nguvu kubwa na nzuri ya kubaki karibu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Kila mara tunafanya makosa kuamini kwamba kama tunatubu sana, basi itakuwa tuko mbali Nao. Lakini kinyume chake ni kweli!

Toba haikuweki mbali Nao—inakuleta karibu zaidi na Wao!

Unaweza kupata kustahili sana kuwa wa mahala fulani na uhusiano wa kina zaidi na Wao kupitia juhudi zako za kuwageukia Wao kwa ajili ya msaada na kupokea msamaha.

Kila mmoja wetu anaweza kuhisi yuko mbali na ukamilifu kuliko ambavyo tungependa, lakini sifikirii kwamba Baba wa Mbinguni analichukulia hilo kwa uzito kama ilivyo hamu yetu na juhudi zetu za kujaribu tena. Yeye anatupenda, Yeye anajua wapi tunakoelekea, na kwa upendo atatuongoza muda wote.

Kukubali madhaifu na makosa yetu kunahitaji mazingira magumu, lakini kwa kutubu, tunamwalika Baba wa Mbinguni kuwa karibu na yale mazingira yetu magumu. Ukaribu ule unamruhusu Yeye kunyoosha upendo Wake mkuu kwetu na kutoa uponyaji, msamaha, na usalama tunaouhitaji. Ni katika muunganiko huu na Mungu ndipo tunakuza kutumainia na kupata kutiwa moyo na kustahili kuwa wa mahala fulani.

Uumbaji

Uumbaji,, na Annie Henrie Nader

Kutafuta Mtazamo wa Juu zaidi

Mtazamo wetu unaweza kuchangia kwenye hisia yetu ya kustahili kuwa wa mahala fulani katika Kanisa la Bwana. Tunaweza kuchagua mtazamo ambapo vitendo vyetu wenyewe vinaweza kuisaidia kata yetu, Muungano wetu wa Usaidizi, au akidi yetu ya wazee kuwa sehemu yenye kupendeza kustahili kuwa wa mahala fulani. Kutafuta kuwasaidia wengine kustahili kuwa wa mahala fulani kwa hakika kunaongeza hisia zetu wenyewe za kustahili kuwa wa mahala fulani.

Kwa sababu wewe ni mtoto wa Mungu, unastahili kuwa wa mahala fulani—bila kujali jinsi wengine wanavyokuona au jinsi unavyoweza kujiona mwenyewe. Mpango wa Baba wa furaha umekusudiwa kwa ajili yako, na wewe una jukumu muhimu la kufanya ndani yake. Kila mmoja wenu ana uwezo kwa kipekee kuchangia na kustahili kuwa wa ufalme wa Mungu, bila kujali hali yako ya ndoa, elimu, au historia.

Wazo ambalo limekuja kwa kujirudia akilini mwangu ni kwamba maneno “vijana wakubwa waseja,” “vijana wakubwa,” na watu wazima waseja” siyo kile ulicho. Haya ni maneno ya kidemografia ambayo yanasaidia kuelezea umri na hali ya ndoa, lakini hayatoshi kuelezea utambulisho wa kweli wa milele, madhumuni, na uwezo.

Vitambulisho, au mifananisho inaweza kuweka ukomo juu ya jinsi tunavyojiona sisi wenyewe na thamani yetu na tunavyoweza kuwa katika ufalme wa Mungu. Ukweli ni kwamba ninyi ni waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Mmefanya maagano na Mungu. Mna njia ya kufikia nguvu Yake ya ukuhani. Wewe ni mshiriki wa Muungano wa Usaidizi au akidi ya Wazee. Wewe ni, kama Rais Nelson alivyofundisha, mtoto wa Mungu, mtoto wa agano, na mfuasi wa Yesu Kristo. Hivyo ndivyo kwa kweli ulivyo kwanza na milele na hicho ndicho kile “kitakachokuongoza kuelekea maisha ya milele katika ufalme wa selestia wa Mungu.”3

Injili ilirejeshwa kupitia nabii mwenye umri wa kijana mkubwa—Joseph Smith. “Hili ni wazo lenye nguvu kulifikiria. Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo walimwamini Nabii na washirika wake katika umri ule kurejesha Kanisa. Mungu pia anakuamini wewe kuwa sehemu ya kazi hii kubwa katika siku hizi za mwisho.

Kama unataka kujua wewe ni nani na kama unapendwa na kuthaminiwa, muulize Baba yako wa Mbinguni. Siku zote atakueleza ukweli kuhusu wewe. Yeye atakusaidia ujione kama Yeye anavyokuona wewe—kwa uwezo mkubwa na upendo. Yeye anaweza kukuongoza kwenye fursa kubwa na ukuaji ambao usingeweza kamwe kuufikiria.

Sisi sote na tuweze kuwa na macho ya kuonana sisi kwa sisi siyo kupitia lenzi ya umri au hali ya ndoa bali kupitia lenzi zinazotuunganisha za washika maagano, wafuasi wenza wa Yesu Kristo, marafiki, akina kaka na akina dada, na wana na mabinti wa Mungu. Na katika majukumu hayo na uhusiano wa milele, tutapata hisia ya juu na ya kweli zaidi ya kustahili kuwa wa mahala fulani.

Muhtasari

  1. Russell M. Nelson, “Agano Lisilo na Mwisho,” Liahona, Okt. 2022, 5.

  2. Russell M. Nelson, “Hekalu na Msingi Wako wa Kiroho,” Liahona,, Nov. 2021, 95–96.

  3. Russell M. Nelson, “Choices for Eternity” (worldwide devotional for young adults, May 15, 2022), Maktaba ya Injili.