“Ni Kweli Zipi Ambazo 1 Nefi na 2 Nefi Zinatufundisha kuhusu Yesu Kristo?,” Liahona, Machi 2024.
Njoo, Unifuate
Ni Kweli Zipi Ambazo 1 Nefi na 2 Nefi Zinatufundisha kuhusu Yesu Kristo?
Karibu na mwisho wa maandishi yake, Nefi anasema, “Kama mtaamini katika Kristo mtaamini katika maneno haya, kwani ni maneno ya Kristo” (2 Nefi 33:10). Kweli nyingi kuhusu sifa za Mwokozi, maisha, na Upatanisho zinapatikana katika kile tulichojifunza katika Kitabu cha Mormoni hadi sasa kwa mwaka huu.
Sifa za Kristo
-
Yeye amejawa na subira, huruma, na uvumilivu (ona 1 Nefi 19:9–6).
-
Yeye siku zote atatukumbuka (ona 1 Nefi 21:14–1).
-
Yeye anamwalika kila mtu aje kwake (ona 2 Nefi 26:24, 33).
Huduma ya Kristo
-
Yeye alifundisha injili Yake na kuwaponya wagonjwa (ona 1 Nefi 11:24, 27–31).
-
Yeye alionesha mfano wa utii kwa kubatizwa (ona 1 Nefi 10:9); 2 Nefi 31:7–12).
-
Yeye alisulubiwa, akazikwa kaburini, na aliwatembelea Wanefi baada ya kufufuka Kwake (ona 1 Nefi 19:10–11; 2 Nefi 26:1).
Upatanisho wa Kristo
-
Yeye alitukomboa kupitia dhabihu Yake (ona 2 Nefi 2:6-7).
-
Yeye alitekeleza “upatanisho usio na mwisho” ambao unashinda kifo cha kimwili na kiroho (2 Nefi 10:5).
-
Yeye anatuwezesha wakati tunapokuwa na imani Kwake na kuchagua kutubu (ona 2 Nefi 31:13).