“Ni Kwa Jinsi Gani Kuwa Mpatanishi Kunanisaidia Niikusanye Israeli?,” Liahona, Machi 2024.
Njoo, Unifuate
Ni Kwa Jinsi Gani Kuwa Mpatanishi Kunanisaidia Niikusanye Israeli?
Nefi aliona kwamba watu katika siku za mwisho wangegombana wao kwa wao (ona 2 Nefi 28:3–4, 20), lakini ugomvi siyo njia ya Bwana. Kwa kweli, kuikusanya israeli tunahitaji kuwa na “njia ya juu zaidi na takatifu zaidi”1 njia ya kuchangamana na wengine.
Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Kama una nia ya dhati kuhusu kusaidia kuikusanya Israeli na kuhusu kujenga uhusiano ambao utadumu milele na milele, sasa ndio muda wa kuweka kando uchungu wote. Sasa ni muda wa kuacha kusisitiza kwamba ni kwa njia yako au la hakuna njia. Sasa ni muda wa kuacha kufanya vitu ambavyo huwafanya wengine wajizuie wakihofia kukukasirisha. Sasa ni muda wa kuzika silaha zako za vita. Kama ghala yako ya maneno imejaa matusi na mashitaka, sasa ni muda wa kuyatupilia mbali. Utainuka kama mwanamume au mwanamke wa Kristo aliye imara kiroho.”2
Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanawapenda watoto wote wa Mungu bila kujali tofauti zao. Shetani anajaribu kutumia tofauti zetu ili kutugawa lakini kwa kuchagua amani kuliko ugomvi, tunajenga mazingira ya kukaribisha ambayo yanawavuta watu kwenye injili ya Bwana iliyorejeshwa.
Fikiria hali zifuatazo na takafari njia unazoweza kujibu kwa upendo.