“Uraibu wa Tamthilia: Jinsi Nilivyomwacha Mungu Ashinde,” Liahona, Machi 2024.
Uraibu wa Tamthilia: Jinsi Nilivyomwacha Mungu Ashinde
Wakati nilipoacha kuangalia mfululizo huu wa tamthilia, nilihisi ushawishi wa Roho Mtakatifu umeongezwa katika maisha yangu vizuri mno.
Kumchagua Yesu Kristo kunaleta nguvu kubwa, “na oh, jinsi gani tutakavyohitaji nguvu Zake siku zijazo.”1 Dunia yetu iko katika vurugu kubwa mno. Adui anaonekana kuwa na ushawishi mkubwa juu ya wengi wa watoto wa Mungu. Uovu unatukuzwa, na majaribu yanatuvuruga mawazo na kutuchukua mbali kutoka kile ambacho kitatuleta karibu zaidi na Bwana.
Kushinda hili lazima kwa nguvu zote tumchague Yesu Kristo ndani ya maisha yetu na kuacha vitu ambavyo vinamchukiza Roho. Moroni alitushauri, “Muwe na hekima katika siku zenu za majaribio, jiondoeni kutoka kwenye uchafu wote” (Mormoni 9:28) na alitualika, “Mje kwa Kristo na mkamilishwe ndani Yake, na mjinyime ubaya wote, … na kumpenda Mungu kwa mioyo yenu, akili, na nguvu zenu”.(Moroni 10:32).
Ni kwa jinsi gani tunaweza kuacha vitu vya kiulimwengu na kwa nia zaidi kuja kwa Kristo? Kila mmoja wetu yupo kwenye kiwango tofauti katika mchakato huu. Sisi sote tunaweza kuacha kitu fulani ambacho kinatuzuia kuhisi ushawishi wa Roho Mtakatifu kwa ukamilifu zaidi. Tunahitaji nguvu za Upatanisho wa Mwokozi ili kufanya hivyo, na inaanza na kutumia haki yetu ya kujiamulia kumchagua Yeye.
Tamaa ya Kukubalika
Nilipokuwa mkubwa katika shule ya upili, nilikuwa katika timu ya ushangiliaji ya chuo kikuu. Kila siku kwenye mazoezi, wasichana kwenye timu yangu ya ushangiliaji walizungumza kuhusu nini kilikuwa kinaendelea kwenye mfululizo wa tamthilia katika muda wa mchana kwenye runinga. Nilikuwa kamwe sijawahi kuingalia na kujua kwamba ilikuwa maonyesho yenye maadili ya chini. Hata hivyo, nilihisi kuachwa nje kila siku wakati wa mazoezi wakati wasichana kwa furaha wakizungumza kuhusu maonyesho hayo. Roho alininon’goneza kutokuiangalia lakini nilifanya jaribio la mwisho kutaka kujumuishwa katika mazugumzo yao, kwa hiyo nilianza kuiangalia.
Haikuonekana mbaya sana kwangu. Nilihalalisha kwamba isingeniathiri. Nilijua kwamba sikuwa nikifanya vitu vibaya ambavyo niliviona wahusika wakifanya. Nilikamatwa na niliangalia maonyesho haya kila siku. Nilipokwenda chuo kikuu cha Brigham Young nilipanga ratiba ya darasa langu ili niweze kuyaangalia kila siku. Kamwe sikukosa mfululizo hata mmoja.
Niliolewa na nilipata mtoto wangu wa kwanza. Ninamweka kwa ajili ya kulala kidogo kila siku wakati wa maonyesho ili niweze kuyaangalia.
Miaka ilipokuwa inapita, Roho alininong’oneza mara nyingi kwamba napaswa kuacha kuangalia maonyesho yale. Lakini nilikataa. Nilijihusisha mno na wahusika na maisha yao. Ilikuwa njia yangu ya kupumzika, kwa hiyo niliendelea kuangalia. Nilikuwa nimeamini kwamba haikuwa inaniumiza.
Mwaliko
Miaka kumi na tisa baada ya shule ya upili, nilikuwa bado naangalia maonyesho hayo kila siku. Wakati wa mkutano mkuu, Dada Sheri L. Dew, wakati huo mshauri wa Pili katika Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi, alikuwa akizungumza kuhusu kujiondoa kutoka ulimwenguni na kwenye vitu ambavyo siyo vitakatifu. Kisha alisema, “Ninamwalika kila mmoja wetu atambue angalau kitu kimoja tunachoweza kufanya ili kuondoka nje ya ulimwengu na kumsogelea Kristo.”2
Wakati alipotoa mwaliko ule, nilihisi mmiminiko wa ajabu wa Roho, na nilisikia maneno katika akili yangu, “Unatakiwa kuacha kuangalia maonyesho hayo sasa!” Mwaliko ulikuwa na nguvu sana; ulikuwa kama kofi usoni kwangu. Nilijua mara ile kwamba sikupaswa tena kupuuza ushawishi huu. Nilihisi ulazima wa kutoangalia maonyesho haya tena. Nilitambua kwamba hakuna mhusika hata mmoja aliyekuwa akifanya chochote chenye uadilifu au heshima. Nilikuwa naalika takataka ndani ya maisha yangu kila siku. Niliahidi kwa Bwana, wakati ule na pale pale, kwamba kamwe nisingeangalia tena.
Haikuwa rahisi! Miaka kumi na tisa ya tabia na urahibu ilikuwa ngumu kuivunja. Jumatatu ilifika na ulikuwa muda wa maonyesho kuanza. Nilikwenda kwenye rimoti ya TV. Nilitaka sana kuiwasha. Nilikumbuka ahadi yangu kwa Bwana kwamba nisingeyaangalia wakati wowote tena. Niliachana nayo.
Kisha niliwaza kuhusu mhusika wangu ninayempenda na kuwaza nini kimeweza kumtokea na nilirudi kwenye rimoti. Nilijua nilihitaji msaada wa Mungu, kwa hiyo nilipiga magoti na nilisali kwa ajili ya nguvu kuweza kuacha kuyaangalia. Nilifikiria ahadi yangu kwa Baba wa Mbinguni, na nikaondoka chumbani. Nilichagua kufuata ushawishi niliopokea kutoka kwa Roho Mtakatifu na kuheshimu ahadi yangu.
Mpangilio ule wa maonyesho ulijirudiarudia kila siku wiki ile na mpaka iliyofuata. Kila siku, nilipiga magoti na kusali na nilisihi kwa ajili ya nguvu za kutoyaangalia, na kila siku nilimchagua Yesu Kristo na niliondoka kwenye maonyesho ya runinga ambayo hayakuwa na maadili. Nilipokea nguvu ya kushinda kutokana na uwezo wa Mwokozi anaotoa kupitia Upatanisho Wake.
Baada ya muda kidogo wa kufanya hivi, muujiza ulitokea. Nilipoteza kabisa hamu ya kuangalia maonyesho yale, baada ya kuyaangalia kila siku kwa miaka 19. Ilikuwa ya kustaajabisha! Pia nilipoteza hamu ya kuangalia maonyesho yote yenye mashaka niliyokuwa nayaangalia, kwa hiyo niliacha kabisa.
Dhamiri yangu ikawa imeamshwa, na nilitambua uovu kwa kile hasa ulichokuwa. Kwa uaminifu nilitaka kujitenga na ubaya wa kila namna (ona 1 Wathesalonike 5:22). Sikuwa mkata tamaa tena.
Baraka ya Ajabu Zaidi
Lakini kitu cha ajabu mno ambacho kilitokea kilikuwa kwamba nilihisi ushawishi wa Roho Mtakatifu umeongezwa katika maisha yangu zaidi ya chochote nilichokuwa na uzoefu nacho kabla. Maendeleo yangu ya kiroho yaliongezeka kasi vizuri mno! Miaka yote hiyo nilikuwa nimedhani nilifurahia wenza wa Roho Mtakatifu, lakini nimekuwa nikipata uzoefu tu wa kipande chembamba cha kile ambacho ningepata. Nilitambua kwamba kuangalia maonyesho hayo muda ule wote kuliniathiri. Nilikuwa nimepoteza miaka mingi mno ya kuwa na wenza wenye nguvu na Mungu. Wakati nilipotumia haki ya kujiamulia ili kuacha uovu, vitu vya kiulimwengu, Roho alikuwa huru kuja kwangu kwa kiasi kikubwa zaidi, na ni tofauti ya ajabu kubwa ambayo imefanyika ndani yangu ili kuniimarisha, kunipa faraja, na kuniongoza.
Tunapenda kushikilia kwa nguvu zaidi vitu visivyo na thamani—vitu ambavyo kwa kweli vinafanya mlango kufungwa kwa baraka ambazo Mungu anataka kuleta ndani ya maisha yetu. Kwa nini tunabadilisha ushawishi wenye nguvu sana unaowezesha wa Roho kwa burudani au kitu maarufu? Labda kuangalia maonyesho ya runinga siyo jambo kubwa au dhambi kubwa mno, lakini iliniweka kutoka kuwa na Roho Mtakatifu kwa wingi mno katika maisha yangu na kupunguza sana maendeleo yangu ya kiroho.
Nina shukrani sana kwamba Bwana hakuniacha bali kwa subira aliendelea kuniomba niache kitu fulani kiovu ili Yeye aweze kujaza maisha yangu mpaka yafurike kwa ushawishi Wake.
Mwandishi anaishi Utah, Marekani.