Kile Nilichogundua Wakati Nilipojitenga na Mitandao ya Kijamii,” Liahona, Machi 2024.
Kile Nilichogundua Wakati Nilipojitenga na Mitandao ya Kijamii
Kupunguza matumizi ya mitandao yangu ya kijamii kumeniruhusu niwepo zaidi kwa ajili ya watoto wangu na niboreshe uhusiano wangu na Mwokozi.
Kwa miaka kadhaa ya iliyopita, nilijua kwamba Mungu alikuwa ananishawishi nitoke kwenye mitandao ya kijamii. Nilijua kwamba mapumziko kutoka kwenye mitandao ya kijamii yalikuwa kitu kizuri kwangu, lakini pia nilijua kwamba nilifurahia jamii ambayo nilikutana nayo huko. Sijui jinsi ya kupatanisha vitu hivi viwili, nilijua tu kwamba kitu fulani kimebadilika.
Nilisoma kitabu ambacho kilinisababisha nitafakari swali, “Ni muda kiasi gani kwenye mitandao ya kijamii ndiyo kiasi sahihi kutoa faida kwenye jamii, bila vishawishi vyote hasi?” Kwangu mimi, jibu kwa swali hili lilikuwa takribani dakika 20 … kwa mwezi. Niliweka lengo kufanya hili liwezekane, na kwa msaada wa Bwana, ilikuwa rahisi mno kuliko nilivyofikiria. Kitu ambacho sikukitegemea kilikuwa kwa kiasi gani mabadiliko haya yangeimarisha uhusiano wangu na Mwokozi wangu. Nilikuja kuhisi vyema upendo ambao Mwokozi anao kwangu, nimekuja kuelewa kwa uwazi zaidi mpango alionao kwa ajili yangu, na nimekuja kuona mahitaji ya watu wanaonizunguka kwa uwazi zaidi.
Bila Kuacha Selfies Ziamue Thamani Yangu Binafsi
Nimejua siku zote kwamba mimi ni mwana wa Mungu na kwamba Yeye ananipenda. Nimesikia upendo wa Mwokozi wangu wakati wa nyakati ngumu katika maisha yangu. Lakini mara nyingi nilikuwa naiachia mitandao ya kijamii iamuru jinsi nilivyojiona na kujifikiria mwenyewe. Kadiri nilivyojaribu kujishawishi mwenyewe kwamba picha za kinadharia kwenye mitandao ya kijamii hazikuniathiri, ilitokea kwamba ziliniathiri. Kupunguza muda wangu kwenye mitandao ya kijamii kuliruhusu amani ya akili na ukimya ambao niliuhitaji ili kumsikia Mwokozi akiniambia jinsi alivyohisi kuhusu mimi. Sikutambua kiasi gani nilikuwa nimekosa kuisikiliza sauti Yake mpaka nilipotengeneza nafasi zaidi kwa ajili Yake kuwa pale.
Siku zote nimekuwa ninaamini katika mpango wa wokovu. Najua kwamba Yesu Kristo ni kiini cha mpango huo. Lakini pia ninaamini kwamba Baba wa Mbinguni anao mpango kwa ajili ya kila mmoja wetu binafsi. Larry M, Gibons, Mshauri wa Kwanza wa zamani katika Urais Mkuu wa Wavulana, alifundisha “Ninajua kwamba Baba wa Mbinguni anajishughulisha kuhusu kila mmoja wetu binafsi na ana mpango binafsi kwa ajili yetu tuweze kutimiza majaliwa yetu ya milele.”1
Nilitumia muda mwingi sana kutafuta ili kujaribu kuelewa nini lilikuwa kusudi langu. Kuwa kwenye mitandao ya kijamii kulinipa kiti kwenye mstari wa mbele kwenye ubunifu wote, vitu vya kustaajabisha watu walivyokuwa wanafanya. Nilijifunza mengi kutoka kwa watu hawa, lakini nilitumia muda mwingi zaidi kutafuta kuliko kufanya. Tangu niondoke kwenye mitandao ya kijamii nimehisi kuongozwa kujua kile hasa ambacho Baba wa Mbinguni atataka mimi nifanye. Vingi kwenye vitu hivi vimekuwa vya kushangaza na tofauti kutoka kwenye vile nilivyodhani vingekuwa, lakini vimeyafanya maisha yangu yawe na utajiri na wingi zaidi.
Mwokozi alikuja ili tuwe na uzima kisha tuwe nao tele (ona Yohana 10:10). Nina shukrani kwa miguso ambayo Roho Mtakatifu anatoa kwetu ili kutusaidia tuwe na maisha tele zaidi.
Maisha zaidi ya Skrini
Mwokozi aliwaona wale ambao hawakutambuliwa na wengine. Ninapenda kusoma hadithi kuhusu Yeye kuhudumia kwa watu kama hao na kuwafundisha thamani yao. Kutumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii kwa kweli kulinizuia kuwaona watu katika maisha yangu mwenyewe, ikijumuisha familia yangu. Nilitambua kwamba kama watoto wangu hawakuwa wakihisi nikiwaona, basi punde wangekuwa wakitazama vyanzo vya nje ili kuthibitisha thamani yao.
Nimeshangazwa na upendo ambao ninao kwa watoto wangu kadiri ambavyo nimekuwa pamoja nao. Nimependa zaidi jukumu langu kama mama mwaka jana kuliko hata hapo kabla. Nimekuja kuwajua majirani na nimekuwa nikishiriki kikamilifu zaidi katika jumuia yangu. Fursa zangu kwa ajili ya huduma zimeongezeka. Nilifikiri kwamba mitandao ya kijamii ilikuwa inanisaidia niwe zaidi mwenye ufahamu lakini kiuhalisia sikuwa naishi katika muda wa kutosha kuona kwa uhalisia mahitaji ya wale wanaonizunguka.
Kupunguza matumizi yangu ya mitandao ya kijamii kulionekana kama kitu kidogo na cha kawaida, lakini kimeniruhusu kuongeza sana imani yangu na kuboresha uhusiano wangu na Mwokozi wangu. Ninajua kwamba Baba wa Mbinguni anatupenda, ana mpango kwa ajili yetu na ana watoto wanaohitaji kuhisi kuonwa na sisi vilevile.
Mwandishi anaishi New York, Marekani.