Liahona
Jakarta, Indonesia
Machi 2024


“Jakarta, Indonesia” Liahona, Machi 2024.

Kanisa Liko Hapa

Jakarta, Indonesia

ramani ikiwa na duara kuzunguka Indonesia
mtaa ndani ya Jakarta

Mnamo mwaka 1970 wamisionari sita wa kwanza kuingia Indonesia waliwabatiza waumini wa kwanza, walianzisha mkusanyiko wa kwanza na walianza mchakato kwa ajili ya kutambuliwa rasmi kwa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Mikusanyiko zaidi ya waumini ilianzishwa, na makao makuu ya misheni yalianzishwa huko Jakarta mnamo mwaka 1975. Leo, Kanisa Indonesia lina:

  • Waumini 7,560 (kwa makadirio)

  • Vigingi 2, kata na matawi 24, na misheni 1

  • Hekalu 1 lililotangazwa (Jakarta)

Kujiandaa kwa ajili ya Hekalu

Akina Wantolo kutoka Tangerang, Indonesia waliunganishwa kama familia katika Hekalu la Manila Ufilipino mwaka 2010. Dada Wintolo anasema, “Furaha ilioje tuliyokuwa nayo wakati nabii wetu mpendwa alipotangaza kwamba kutakuwa na hekalu Indonesia. Tutaendelea kusali na kujiandaa wenyewe kwa ajili ya uwepo wa nyumba ya Bwana ndani ya nchi yetu.”

familia ikiwa imesimama pamoja

Picha kwa hisani ya familia ya Wintolo

Zaidi kuhusu Kanisa huko Indonesia

  • Mwaka 1815 mlipuko wa volkano huko Indonesia kwa kweli ulisababisha kwa sehemu Urejesho wa injili. Mzee Quentin L. Cook anaeleza.

  • Kijana kutoka Indonesia “anatumika kama” somo juu ya tumaini.

  • Rais Mkuu wa Zamani wa Muungano wa Usaidizi Linda K. Burton anavutiwa na wanawake wenye imani huko Indonesia.

  • Mwandishi huyu kutoka Indonesia anashiriki Ishara 10 kwamba wewe kwa kweli umeongoka kwenye injili ya Yesu Kristo.

  • Kitabu cha Mormoni, Mafundisho na Maagano, na Lulu ya Thamani Kuu vikawa vinapatikana kama seti Indonesia mnamo mwaka 2010.

Wamisionari wakizungumza na mwanamume mtaani.

Wamisionari wakisalimiana na watu mitaani

Wavulana wa Msingi wakiimba

Watoto wa Msingi wanakusanyika kuimba huko Tangerang Indonesia.

familia imekusanyika nje

Familia ikitumia muda mzuri pamoja nje.

mvulana akipitisha sakramenti kwa waumini

Waumini wanafanya upya maagano yao ya ubatizo kwa kushiriki sakramenti huko Tangerang, Indonesia.