Njia Kumi za Kujua Kuwa Umeongoka
Tyler Orton anaishi Java, Indonesia.
Nilijifunza katika mkutano wa ukuhani kwamba moja ya malengo ya Ukuhani wa Haruni ni kutusaidia “kuwa waongofu kwa injili ya Yesu Kristo na kuishi kwa mafundisho yake.”1 Nilikuwa sina uhakika wa nini maana ya “kuwa waongofu kwa injili ya Yesu Kristo.” Niliwauliza wazazi wangu na ndugu wakubwa kile walichofikiria inamaanisha, na pamoja tulijadili idadi ya njia unaweza kuona kama unakuwa umeongoka.
Pengine kuna zingine, lakini hapa kuna njia 10 tulizotunga. Kwa vile uongofu ni mchakato wa muda wote wa maisha, si lazima tuwe wakamilifu katika kila sehemu hizi sasa, lakini inaweza kutusaidia kujua kama tunafanya maendeleo.
-
Wakati umeongolewa, wewe haujui tu nini unatakiwa kufanya lakini pia una hamu ya kufanya mambo sahihi. Haitoshi tu kuepuka kufanya makosa kwa sababu una hofu ya kupatikana au kuadhibiwa. Wakati kweli umeongolewa, kweli unataka kuchagua mema.
-
Ishara nyingine ya kuwa mwongofu ni kwamba hauna hamu tena ya kufanya makosa. Wapinga-Nefi-Walehi ni mfano mzuri wa hivi. Walipokuwa waongofu kwa Injili ya Kristo, “waliingia kwenye agano na Mungu kwamba watamtumikia, na kutii amri zake” (Mosia 21:31). Kama Wanefi waliofundishwa na Mfalme Benyamini, walikuwa “hawana tamaa ya kutenda maovu” (Mosia 5:2). Walikuwa kweli wameongolewa kwa Injili ya Kristo, na majaribu ya Shetani hayakuwa na nguvu juu yao.
-
Wakati umeongolewa, unajihusisha zaidi na nini Mungu anafikiria kuliko kile wengine wanafikiria juu yako. Shuleni mwangu kule Indonesia, wanafunzi huwa wanakunywa sana. Wakati mwingine inaweza kuwa jaribio kwenda kwa burudani wakati kila mtu anafanya vile na kukukejeli kwa kukosa kuenda. Ndugu yangu alialikwa kunywa na kuburudika mara nyingi, lakini kamwe hakukubali—alisimama kwa ajili ya kile alichoamini. Ilikuwa vigumu, na alibaki usiku mara nyingi nyumbani peke yake. Wakati wanafunzi walikuwa wakimuaga katika mahafali yake, watu kadhaa walishiriki naye jinsi walivyoshangazwa kuwa aliweza kupinga shinikizo ya rika na kuwa mkweli kwa viwango vyake. Walimwambia jinsi walimtazamia kwa sababu ya hivyo. Alionyesha kuwa ameongolewa kwa kukataa shinikizo ya rika.
-
Unapoongolewa, unajaribu uwezavyo kuishi Injili daima—si tu Jumapili au wakati ni rahisi lakini wakati wote. Matendo yako hayabadiliki kulingana na yule ambaye uko pamoja naye au yule ambaye anaweza kuwa anakutazama. Wenzako wanaposema mambo mabaya au wanataka kutazama sinema chafu, haukubali tu kwa sababu hakuna anayekuangalia; badala yake unasimama kwa kile unachoamini.
-
Wakati umeongolewa, una zaidi ya wema na huruma katika uhusiano na watu wengine. Hauhukumu, wala hukosoi, wala umbeya. Una ufahamu zaidi ya hisia za wengine, na inakuwa ni kawaida kutafuta njia za kuhudumu na kusaidia. Ukiwa unatembea chini ya ukumbi wa shule yako na mtu aangushe vitabu vyake, si lazima hata ufikirie juu ya nini cha kufanya. Unasimama moja kwa moja kusaidia.
-
Wakati umeongolewa, hamu yako ya kuomba huongezeka na unahisi kama unawasiliana kwa kweli na Mungu unapoomba. Daima utatenga muda wa kuomba bila kujali jinsi unavyojisikia au kile kinachoendelea katika maisha yako. Rais Ezra Taft Benson (1899–1994) alituambia, “Kama hatuhisi kuomba, basi tunapaswa kuomba hadi tuhisi kuomba.”2
-
Wakati umeongolewa, unatamania Jumapili kwa sababu ni Sabato. Jumapili inapofika, badala ya kufikiri, “Eh, ni siku ambayo siwezi kufurahia na marafiki zangu au kwenda sinema, unafikiri, Vizuri, siku ambayo ninaweza kuhudhuria kanisa na kuzingatia mambo ya kiroho na kufurahia muda na familia yangu!”
-
Wakati umeongolewa, unatii amri na hautafuti sababu, kurazinisha tabia, au kujaribu kupata maeneo yasiyowazi. Haujaribi kusongeza mipaka; unatii amri tu kwa sababu unajua ndiyo njia bora zaidi.
-
Wakati umeongolewa, unatamania kulipa sadaka yako. Unaiona kama upendeleo na kuhisi kwamba asilimia 10 si kwamba ni nyingi, hasa ikilinganishwa na baraka na kuridhika unakopata. Baraka hizi zina thamani ya zaidi kuliko fedha ulizolipa.
-
Wakati umeongolewa, una hamu kubwa ya kuwasaidia wengine kujua ukweli na furaha ambayo umepata. Mfano mzuri kutoka kwa maandiko ni ndoto ya Lehi, ambapo yeye alikuwa na hamu ya nguvu ya kushiriki tunda lenye ladha la mti wa uzima na familia yake. Alipokula tunda, wazo lake la kwanza halikuwa kula zaidi kwa ajili yake mwenyewe lakini kutafuta familia yake ili waweze pia kula tunda na kuwa na furaha sawa (ona 1 Nefi 8:12).
Kwa muhtasari, unajua kuwa umeongolewa unapoanza kuishi sheria ya juu, injili ya Yesu Kristo. Unaishi kulingana na madhumuni ya sheria na pia sheria ilivyoandikwa. Unaishi injili katika nyanja zote za maisha yako. Unaishi injili kwa ukamilifu wake, si kwa sababu unalazimika lakini kwa sababu unataka. Wewe ni mtu mwenye furaha na mwema zaidi, na unataka kuwa mtu ambaye Baba wa Mbinguni anataka uwe. Unataka kuwa kama Yesu Kristo na kufuata mfano Wake. Unapokuwa mtu huyo, kwa kweli umeongolewa.