Daftari ya Mkutano wa Aprili
Kujifunza Hotuba za Mkutano Mkuu Pamoja
Greg Batty anaishi Utah, USA.
Kubadilisha njia yetu ya kurejelea mkutano kuliimarisha zaidi majadiliano yetu ya injili kama familia.
Kwa miaka tumefurahia kusoma kwa kupitia toleo la mkutano kama familia, makala moja kwa wakati tulipoanza, tulikusanyika mezani tu na kwa zamu tulisoma kila mmoja aya kwa sauti. Lakini tuligundua kuwa tulikuwa tukisoma ili kuipitia, bila kutua ili kuelewa ujumbe.
Ili kupata zaidi kutoka kwa kile tulichokuwa tukisoma, mke wangu nami tulinunua nakala moja ya toleo la mkutano kwa kila mwana familia na tukapanga mazungumzo mangapi tungefaa kujifunza kila wiki ili tuweze kuyasoma yote kabla ya mkutano mkuu ufuatao. Wiki kadha tungesoma hotuba moja, na wiki zingine ingekuwa mbili, lakini kila mtu alifaa kusoma hotuba na kuweka alama katika sehemu walizopenda. Kisha kwa Mkutano wa Jioni wa familia nyumbani tungefundishana kutoka kwa sehemu tulizoweka alama.
Mara nyingi watoto wetu walikuwa na maswali yaliyofungua majadiliano yetu, au mke wangu nami tuliuliza maswali kutoka kwa masomo yetu. Tulidhamini kusikia vijana wetu wakieleza majibu yao ya maswali hayo, wakishiriki vitu walivyojifunza katika seminari kanisani, au katika masomo yao ya kibinafsi. Hii ikawa njia nzuri ya kusikiliza shuhuda zisizo rasmi za kila moja mara kwa mara katika mazingira ya starehe na utulivu.
Punde tuligundua kuwa masomo yetu ya maandiko ya asubuhi yalichukua toni sawa. Baadhi ya siku tulipitia mistari michache tu kabla wakati kuyoyoma kutoka kwa mjadala kuhusu mistari hiyo na jinsi ililingana na yale yaliyokuwa yakitendeka karibu nasi.
Asubuhi zetu sasa zimejawa na mazungumzo, vicheko, na umoja kabla ya kila moja wetu kwenda nje kwa shughuli zetu binafsi. Tuna ushuhuda imara wa ushauri ya nabii wetu wa kujifunza na kuomba pamoja kila siku. Familia yetu imebadilishwa kuwa moja ambayo inajifunza kutoka kwa na kuimarishwa kila mmoja. Yote haya ni matokeo ya kutaka kupata zaidi kidogo kutoka kwa mkutano mkuu.