Ujumbe wa Urais wa Kwanza
Amefufuka
Ushuhuda wa ukweli wa Ufufuo wa Yesu Kristo ni chanzo cha matumaini na azimio. Na inaweza kuwa hivyo kwa mtoto yeyote wa Mungu. Ilikuwa kwangu mimi siku moja katika majira ya joto ya Juni 1969 wakati mama yangu alifariki, imekuwa miaka mingi tangu, na itakuwa hadi nimuone tena.
Huzuni kutoka kwa kutengwa kwa muda ilibadilishwa punde kuwa furaha. Ilikuwa zaidi na tumaini kwa ajili ya muungano wa furaha. Kwa sababu Bwana amefunua mengi kupitia manabii Wake na kwa sababu Roho Mtakatifu amenidhibitishia ukweli wa Ufufuo, ninaweza kuona katika mawazo yangu vile itakavyokuwa kuungana na wapendwa wetu waliotakaswa na kufufuka:
“Hawa ndio wale watakaotoka katika ufufuo wa wenye haki.
“Hawa ndio wale ambao majina yao yameandikwa mbinguni, mahali ambako Mungu na Kristo ni waamuzi wa wote.
“Hawa ndio wale watu wenye haki waliokamilishwa kwa njia wa Yesu aliye mpatanishi wa agano jipya, aliye kamilisha upatanisho huu makamilifu kwa njia ya umwagikaji wa damu yake yeye mwenyewe” (M&M 76:65, 68–69).
Kwa sababu Yesu Kristo alivunja minyororo ya kifo, watoto wote wa Baba wa Mbinguni wanaozaliwa duniani watafufuka katika mwili ambao daima hautakufa. Kwa hivyo ushuhuda wangu na wako wa ukweli huo mtukufu unaweza kutoa uchungu wa kupoteza mwanafamilia mpendwa ama rafiki na kubadilisha kwa furaha ya kutarajia na azimio imara.
Bwana ametupa sisi sote zawadi ya ufufuo, ambapo roho zetu zinawekwa katika miili iliyo bila upungufu wa kimwili (ona Alma 11:42–44). Mama yangu ataonekana kuwa kijana na aking’aa, matokeo ya umri na miaka ya mateso ya kimwili yakiwa yametolewa. Hio itamjia yeye na sisi kama zawadi
Lakini wale wetu wanaotamani kuwa naye milele lazima wafanye chaguo kustahili kwa ajili ya uhusiano huo, kuishi ambapo Baba na Mwanawe Mpendwa aliyefufuka wanaishi kwa utakatifu. Hapo ndipo mahali pekee ambapo maisha ya familia yanaweza kuendelea milele. Ushuhuda wa ukweli huo umeongeza dhamira yangu ya kuhitimu mwenyewe na wale ninaowapenda kwa kiwango cha juu kabisa cha ufalme wa selestia kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo ukifanya kazi maishani mwetu (ona M&M 76:70).
Bwana anatupa mwongozo katika jitihada hii ya uzima wa milele katika maombi ya sakramenti yanayonisaidia na yanaweza kukusaidia. Tunaalikwa kufanya upya maagano yetu ya ubatizo katika kila mkutano wa sakramenti.
Tunaahidi daima kumkumbuka Mwokozi. Nembo na dhabihu Yake zinatusaidia kufahamu ukubwa wa thamani aliyolipa Yeye ili kuvunja minyororo ya kifo, kutupatia rehema, na kutoa msamaha wa dhambi zetu zote tukichagua kutubu.
Tunaahidi kutii amri Zake. Kusoma maandiko na maneno ya manabii waliohai na kusikiliza wanenaji wanaoongozwa katika mikutano yetu ya sakramenti kunatukumbusha maagano yetu kwa kufanya hivyo. Roho Mtakatifu huleta mawazoni mwetu na mioyo amri tunazohitaji zaidi kutii siku hiyo.
Katika maombi ya sakramenti, Mungu huagiza kutuma Roho Mtakatifu kuwa pamoja nasi (ona Moroni 4:3; 5:2; M&M 20:77, 79). Nimeona katika wakati huo kwamba Mungu anaweza kunipa kile kinachohisika kama mahojiano ya kibinafsi. Yeye huleta kwa usikivu wangu kile nimefanya kinachompendeza Yeye, haja yangu kwa ajili ya toba na msamaha, na majina na nyuso za watu Yeye angetaka niwatumikie kwa ajili yake.
Miaka nenda miaka rudi, uzoefu huo unaorudiwa umegeuza tumaini kuwa hisia za upendo na kuleta uhakika kwamba rehema ilifunguliwa kwa ajili yangu na Upatanisho wa Mwokozi na Ufufuo.
Nashuhudia kuwa Yesu ndiye Kristo aliyefufuka, Mwokozi wetu, na mfano wetu kamili na mwongozo wa maisha ya milele.