Kuleta Darasa la Msingi Nyumbani
Yesu Kristo Alirejesha Kanisa Lake katika Siku za Mwisho
Unaweza kutumia somo hili na shughuli hii kujifunza zaidi kuhusu mada ya Darasa la Msingi la mwezi huu.
Fikiria kwenda kutafuta hazina. Ni wapi unaweza kutafuta hazina? Unaweza kuipata vipi? Je, kunaweza kuwa na sanduku la hazina? Ni nini kingekuwa ndani?
Baadhi ya masanduku ya hazina huwa na vito vizuri na sarafu za thamani. Lakini kama washiriki wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, tuna hazina ambayo ni ya thamani zaidi: Injili ya Yesu Kristo.
Watu wengi hawajui kuhusu hazina hii, kwa hivyo mojawapo wa majukumu yetu ni kuishiriki na watu wengi iwezekanavyo.
Baada ya Yesu na Mitume wake kufa, baadhi ya mafundisho muhimu ya injili na maagizo yalipotea au kubadilishwa, ikiwa ni pamoja na ubatizo, mamlaka ya ukuhani, mahekalu, manabii hai, na sakramenti.
Hazina hizi zote za injili zilirejeshwa kupitia Nabii Joseph Smith. Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo walimtoekea Joseph Smith katika Msitu Mtakatifu alipoomba kujua ukweli.
Baadaye Joseph alipata mabamba ya dhahabu na kuyatafsiri kuwa Kitabu cha Mormoni. Kitabu cha Mormoni kina mafundisho tunayothamini kwa sababu kinaelezea kweli ambazo awali zilikuwa zimepotea. Tunapokea baraka nyingi kwa sababu tuna kweli hizi za injili.
Ni hazina za thamani jinsi gani!