2013
Kifo na Maisha: Mitazamo ya Watangulizi juu ya Ufufuo.
Aprili 2013


Kifo na Maisha

Mitazamo ya Watangulizi juu ya Ufufuo.

Waongofu wa kwanza wa Kanisa waliposafiri magharibi mwa Merikani kukusanyika na Watakatifu, walikumbana na kifo lakini walistihimiliwa na imani yao mpya katika injili ya urejesho. Yafuatayo ni nukuu kutoka kwa maelezo ya watangulizi yanayoonyesha tumaini la Watakatifi katika Ufufuo, pamoja na mafundisho kutoka kwa Marais wa tano wa kwanza wa Kanisa.

Robert Aveson, akirejelea hadhithi ya baba Msandinavia Mtakatifu wa Siku za Mwisho asiyetajwa ambaye mwanawe alifariki safarini kutoka New York hadi Utah mnamo 1866:

“Na usaidizi wa rafiki kaburi dogo lilichimbwa na mabaki yakawekwa pale ndani. Mtoto aliyefariki kutokana na ugonjwa unaoambukizwa, hapakuwa na waombolezaji, hamnasherehe rasmi, hamna nembo za maua, hamna wimbo wa kiroho, hamna neno la taabini. Lakini kabla ya baba aliyefiwa kuondoka alitamka maombi fupi ya kuweka wakfu katika lugha yake ya asili (Kidenishi) kama ifuatavyo: …

Baba wa Mbinguni: Wewe ulinipa hazina hii ndogo—mvulana huyu mpendwa, na sasa wewe umemuita. Tafadhali ruhusu kwamba mabaki yake yabaki hapa salama mpaka asubuhi ya ufufuo Mapenzi yako yatimizwe Amina.’

“Na akiamuka kutoka ardhini maneno yake yakuaga yalikuwa:

“‘Kwaheri, mpendwa wangu mdogo Hans—mwanangu mzuri.’ Kisha kwa kichwa legevu na moyo wa kuuma alishika njia yake kwa kambi yake.”1

Rais Joseph Smith (1805–44):

“Ni jambo la kuliwaza kwa waombolezaji wanapoitwa kuwachana na mume, mke, baba, mama, mtoto, au ndugu mpendwa, kujua kwamba, ingawa mwili wa kidunia umewekwa chini na kuharibiwa, watafufuka tena kukaa katika mafukizo ya milele katika utukufu wa milele, si kuhuzunika, kuteseka, au kufa tena, bali watakuwa warithi wa Mungu na warithi pamoja na Yesu Kristo.”2

Joseph Watson Young (1828–73), mpwa wa Brigham Young ambaye alisafiri kutoka Uingereza hadi Marekani mnamo 1853:

“Ilikuwa tokeo la ombolezo kufungia kiumbe mwenzagu kwa kimya cha kina saa la kiza la usiku na mashahidi wachache tu wapweke. Hakuwa na jamaa pamoja naye au mtu yeyote hasa wa kuomboleza isipokuwa mtumishi mwenzake. Haya ni matumaini ya furaha ya asili ya binadamu yakiangamizwa kwa masaa. Kijana huyu alikuwa amewacha yote ili kuende katika Sayuni, na moyo wake ulichomwa na matarajio hai ya usoni, kufikiria kidogo kwamba angefungia mwili wake wa kidunia kwa wimbi la njaa. Hata hivyo, alikufa si kama wale wasio na matumaini, kwa kuwa amani yake ilifanywa kwa Mungu wake, na alikuwa na uhakika kamili wa ufufuo mtukufu asubuhi wa wenye haki”.3

Rais Brigham Young (1801–77):

“Jameni bonde la giza na kivuli tunayoita kifo! Kupita kutoka hali hii ya kuwepo mbali na mwili wa kidunia inahusika, katika hali ya udhaifu [utupu], ya ajabu jinsi gani. Kiza jinsi gani bonde hili. Ajabu jinsi gani barabara hii, na lazima tuisafirie peke yetu. Nangependa kuwambieni nyinyi, rafiki na ndugu zangu, kama tungeweza kuona mambo kama yalivyo, na kama tutakavyoyaona na kuyaelewa, kivuli hiki cha giza na bonde ni jambo dogo kwamba tutageuka na kulitazama na kufikiri, wakati tumelivuka, kwa nini hii ni faida kubwa ya kuwepo kwangu kote, kwa maana nimepita kutoka hali ya huzuni, ghamu, msiba, ole, taabu, dhiki na maumivu, na kukata tamaa hadi katika hali ya kuwepo, ambapo ninaweza kufurahia maisha kwa kiwango kikamilifu kabisa hadi panapowezekana kufanyika bila mwili.”4

Dan Jones (1811–62), mwongofu wa Kiwelishi ambaye, pamoja na Bi. Williams na washiriki wengine wa Kanisa, alipanda meli kwenda Marekani mnamo 1849:

“Bi. Williams, wa Ynysybont karibu na Tregaron [Wales], amezidiwa haraka, na dalili ni kuwa hataishi kwa muda mrefu. Alisema kuwa heshima ya juu kabisa aliyowahi kupokea ulikuwa kuwa mshiriki wa kanisa la kweli la Mwana wa Mungu, ya kwamba hakukuwa na uoga moyoni mwake kuhusu maisha yajayo na kuwa dini yake sasa imeonyesha nguvu zake zaidi kuliko hapo awali. Aliwashauri wanawe kwa dhati kuendelea kuwa waaminifu hadi kifo ili waweze kupata pamoja naye ufufuo bora. Aliendelea kuwa timamu kupitia usiku, na saa kumi na robo asubuhi ifuatayo roho yake ikaenda kwa amani, na kuacha tabasamu midomoni mwake.”5

Rais John Taylor (1808–87):

“Kunaliwaza vipi kwa wale ambao wanaitwa kuomboleza kupotea kwa wapenzi katika kifo, kujua kwamba tutahusishwa nao tena. Kunatia moyo vipi kwa wote ambao wanaishi kulingana na kanuni za ukweli zilizofunuliwa, pengine zaidi kwa wale ambao maisha yao yametumika vizuri, ambao wamevumilia joto na mzigo wa siku, kujua kuwa kabla ya kuwafikia kwa muda mrefu tutapasua vikwazo vya kaburi, na kutokea roho hai na zisizokufa, kufurahia jamii ya marafiki zetu waliojaribiwa na kuaminiwa, katu kuadhibiwa tena na mbegu ya kifo, na kumaliza kazi ambao Baba ametupa tufanye!”6

Andrew Jenson (1850–1941), Mhamiaji wa Kidenishi ambaye alisafiri katika kundi la mkokoteni la Andrew H. Scott kutoka Nebraska, USA, hadi Utah mnamo 1866:

Tuliposhuhudia mabaki ya kidunia yao [wasafriri wenzetu] yakiwekwa kwenye ardhi, kwenye jangwa, sote tulilia, ama kuhisi kulia; kwa kuwa fikra ya kuzika wapendwa kwa jinsi hii, ambapo marafiki na jamii lazima punde wakimbie kuenda, bila tumaini ya kuwai kutembelea mahala pa kupumzikia pa wapendwa wao walioaga, ilikuwa ya kuhuzunisha na jaribio kweli. Lakini kaburi zao zitapatikana wakati Gabrieli atakapopiga tarumbeta yake katika asubuhi wa ufufuo wa kwanza. Hawa waliooaga basi walilaza miili yao chini walipokuwa wakitembea kuelekea Sayuni. Bwana aliwaita nyumbani kabla wafike walikokuwa wakienda, hawakuruhusiwa kuona Sayuni katika mwili; lakini watapokea utukufu na kufurahia hapo baadaye; waliaga wakijitahidi kutii Mungu na kutii amri zake, na wabarikiwa ni wale wanaokufa katika [Bwana].”7

Rais Wilford Woodruff (1807–98):

“Bila injili ya Kristo utengano kwa kifo ni mojawapo wa mada ya kuhuzunisha kabisa ya kutafakari; lakini punde tu tunapopokea injili na kujifunza kanuni za ufufuo huzuni, dhiki, na mateso yanayoletwa na kifo yanaolewa, kwa kiwango kikubwa. Ufufuo wa waliokufa unajitokeza mbele ya akili iliyoelimika ya mwanadamu, na hana msingi wa roho wake kulalia. Huu ndio msimamo wa Watakatifu wa Siku za Mwisho hata leo. Tunajijulia, hatuko gizani katika swala hili, Mungu ametufunulia na tunaelewa kanuni ya ufufuo wa waliokufa, na injili huleta uzima na kutokufa kwa ufahamu.”8

William Driver (1837–1920), mtangulizi aliyesafiri kutoka Uingereza hadi New York, USA, mnamo 1866:

Willie, mtoto wangu mpendwa, alikuwa mgonjwa sana usiku mzima hadi 7:30 asubuhi, alipowachiliwa kutoka kwa mateso yake. Mungu bariki nafsi yake. Jinsi alivyoteseka. Aliaga kupitia mkokoteni wa Bwana Poulter kusimama kwenye mlima wa St. Ann, Wandsworth, Surrey, Uingereza. Eh, jinsi ninavyoomboleza dhiki hii kuu Ewe Bwana, nisaidie kwa uwezo wako kuuvumilia kama kwa mkono wako na nishawishi kukutumikia Wewe kwa ulodi na uaminifu zaidi, na ni weze kuishi ili kujitayarisha kukutana naye katika dunia yenye furaha na bora zaidi na dadake mpendwa, Elizabeth Maryann, na katika ufufuo wa wenye haki niweze kuwa hapo kukutana nao.”9

Rais Lorenzo Snow (1814–1901):

“Katika maisha yafuatayo tutakuwa na miili mitukufu na tutakuwa bila ugonjwa na kifo. Hakuna kilichopendeza zaidi kama vile mtu katika hali ya ufufuo na utukufu. Hakuna kilicho cha kupendeza zaidi kushinda kuwa katika hali hii na kuwa na wake wetu na watoto na marafiki nasi.”10

Muhtasari

  1. Robert Aveson, “Leaves from the Journal of a Boy Emigrant,” Deseret News, Mar 12, 1921, 4:7; inapatikana lds.org/churchhistory/library/pioneercompanysearch.

  2. Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 52.

  3. Joseph W. Young, Journal, Mar. 6, 1853, Church History Library, Salt Lake City, Utah; inapatikana katika mtandao mormonmigration.lib.byu.edu.

  4. Teachings of Presidents of the Church: Brigham Young (1997), 273.

  5. ”Barua Kutoka kwa Nahodha D. Jones kwa mhariri wa Udgorn Seion,” katika Ronald D. Dennis, The Call of Zion: The Story of the First Welsh Mormon Emigration, vol. 2 (1987), 164–65; inapatikana mormonmigration.lib.byu.edu.

  6. Teachings of Presidents of the Church: John Taylor (2001), 50–51.

  7. Andrew Jenson, Journal, Aug. 20, 1866, katika Journal History of The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints, Oct. 8, 1866, Church History Library, Salt Lake City, Utah, 6; inapatikana lds.org/churchhistory/library/pioneercompanysearch.

  8. Teachings of Presidents of the Church: Wilford Woodruff (2004), 82–83.

  9. Frank Driver Reeve, ed., London to Salt Lake City in 1866: The Diary of William Driver (1942), 42; inapatikana mormonmigration.lib.byu.edu.

  10. Lorenzo Snow, katika Conference Report, Oct. 1900, 63.

Kielelezo na Michael T. Malm NA USULI NA Welden C. Andersen © IRI

Kushoto: Rais Brigham Young Juu: Joseph Watson Young.

Kulia: Rais John Taylor. Juu: Dan Jones.

Vipachikwa: Brigham Young, na John Willard Clawson; picha ya Joseph Watson Young, kwa hisani ya Church History Library; picha ya Dan Jones © IRI; John Taylor, na A. Westwood, kwa hisani ya Church History Museum

Kushoto: Rais Wilford Woodruff. Juu: Andrew Jenson.

Kulia: Rais Lorenzo Snow. Juu: William Driver.

Vipachikwa: Wilford Woodruff, na H. E. Peterson © IRI; picha ya Andrew Jenson, na Harold Howell Jenson, kwa hisani ya Church History Library; picha ya William Driver, kwa fadhili ya Church History Library; Lorenzo Snow, na Lewis Ramsey, kwa hisani ya Church History Museum © IRI