Kote Kanisani
Tangazo la Picha za Vijana
Mada ya Mutual mwaka huu ni “Simameni katika mahali pa takatifu na wala msiondoshwe” (M&M 87:8). Wavulana na wasichana, Liahona inatafuta picha zenu mkiwa mmumesimama katika maeneo matakatifu. Picha zinaweza kuonyesha ukiwa na familia, ukihudumu, ukifanya kazi ya umisionari, ukitengeneza sanaa, kusoma Injili, kuchunguza mazingira, na zaidi! Hivi ndivyo unavyotuma picha yako:
-
Acha mtu akupige picha ukiwa umesimama mahali pa takatifu.
-
Tuma picha yako ya ubora wa juu kwa liahona@ldschurch.org.
-
Ongeza ujumbe kuhusu kwa nini mahali hapa ni pa takatifu kwako.
-
Katika barua pepe yako, jumuisha jina lako kamili, siku ya kuzaliwa, jina la kata na kigingi ( ama tawi na wilaya), na anwani ya barua pepe ya wazazi wako.
Picha za vijana kutoka duniani kote zitawekwa katika toleo lijalo.
Mtume Anazuru Morocco
Mnamo Desemba 2012, baada ya kuunda kigingi cha 3000 cha Kanisa kule Sierra Leone Afrika Magharibi, Mzee Jeffrey R. Holland wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili alitembelea tawi dogo la Kanisa lililo mbali kule Rabat, Morocco.
Katika ibada maalum ya Jumapili jioni, Mzee Holland alishiriki upendo ambao viongozi wa Kanisa wanao kwa kila mshiriki wa Kanisa duniani kote, bila kujali jinsi walivyo wachache au umbali wa mahali walipo.
“Hamjasaulika, na ninyi ni sehemu ya kazi ya ajabu kama vile Bwana hubainisha na kuharakisha kukusanyika kwa Israeli katika kipindi hiki kikuu cha mwisho,” alisema.
Hekalu la Tegucigalpa Honduras Liwekwa Wakfu
Jumapili wa Machi 17, 2013, kufuatia sherehe za kitamaduni na wiki tatu za kukaribisha wageni, Hekalu la Tegucigalpa Honduras liliwekwa wakfu katika vikao vitatu, ambavyo vilitangazwa kwa vitengo vyote vya Kanisa katika Honduras na Nicaragua.
Washiriki wa Honduras, ambao kwa kawaida wamekuwa wakisafiri masaa mengi kwenda Guatemala kwa Hekalu la Guatemala Mjini, walifurahi kuona hekalu la kwanza nchini likiwekwa wakfu. Hekalu lilitangazwa kwa mara ya kwanza na Urais wa Kwanza katika barua ya Juni, 9, 2006, na ardhi ilichimbuliwa katika uwanja huo mnamo Septemba 12, 2009.
Rais Monson Azuru Ujerumani
Mwishoni mwa mwaka 2012 Rais Thomas S. Monson alisafiri kwenda Ujerumani kukutana na washiriki wa Kanisa Hamburg, Berlin, Munich, na Frankfurt, Ujerumani, na kuwahimiza wamfuate Yesu Kristo.
Alifunza msamaha kwa njia ya kusamehe, aliwaambia washiriki kule Frankfurt. Alifunza huruma kwa kuwa na huruma. Alifundisha ibada kwa kujitolea Mwenyewe.