2013
Mafunzo ya Uongozi Duniani Kote — Mbinu Mpya
Aprili 2013


Mafunzo ya Uongozi Duniani Kote—Mbinu Mpya

Katika miezi ijayo, washiriki wa Kanisa ulimwenguni watashiriki katika mfumo mpya wa maongozi ya Mafunzo ya Uongozi Duniani Kote.

Tofauti na mikutano ya awali ya mafunzo, Mafunzo ya Uongozi Duniani Kote ya mwaka huu hayatatangazwa kama tukio moja kwa ajili ya viongozi wa kata na vigingi. Badala yake, yatagawanywa katika vipingili tisa vifupi—katika DVD na kwenye LDS.org—ambayo inahimiza majadiliano na viongozi wote, washiriki, na familia mwaka ujao mzima na baadaye.

Lengo la mafunzo ni Kuimarisha Familia na Kanisa kupitia Ukuhani. Katika mafunzo, washiriki wa Urais wa Kwanza na Jamii ya Mitume Kumi na Wawili, pamoja na Viongozi wengine Wenye Mamlaka na maafisa wakuu, wanatoa maelekezo ya kuvutia juu ya:

  • Jinsi familia zinaweza kupata nguvu na amani kupitia uwezo wa ukuhani.

  • Jinsi ya kusaidia kila familia kuwa na uzoefu wa baraka za ukuhani.

  • Jinsi wenye funguo za ukuhani wanaimarisha nyumba na familia.

  • Jinsi ya kushiriki kwa njia za Kikristo

  • Jinsi ya kuwalea watoto katika nuru na ukweli.

Vitengo vyote vya Kanisa vitapokea nakala za DVD, na mabaraza ya kata na vigingi yanaombwa yazitazame kikamilifu. Kisha wanapaswa kushauriana kuhusu jinsi ya kusaidia washiriki wa kata na kigingi kufaidika kutokana na mafundisho.

Katika mikutano na madarasa, washiriki wanaweza kutazama na kujadili vipingili vya DVD. Familia na watu binafsi wanaweza kutazama vipingili, pamoja na nyenzo za ziada ili kuboresha masomo yao, katika wwlt.lds.org.

Katika kila mazingira, sehemu yenye umuhimu zaidi ya mafunzo itatokea baada ya kukamilika kwa kipingili na mjadala kuanza. Viongozi, washiriki, na familia wanapotafakari, kushiriki, na kushuhudia kuhusu walichokisikia na kuhisi, Roho Mtakatifu atawavutia na kuwafundisha jinsi ya kutumia mafundisho katika mazingira yao wenyewe. Kupitia uzoefu huu, Mafunzo ya Uongozi Duniani Kote haya yatasaidia kuimarisha familia na Kanisa duniani kote.

Mzee L. Tom Perry, Mzee Donald L. Hallstrom, na Askofu Dean M. Davies wanaongoza jopo la mjadala juu ya umuhimu wa kutumia funguo za ukuhani.

Wakiwa wamesimama nje ya nyumba ya Mary Fielding Smith katika “This Is the Place Heritage Park”, Mzee M. Russell Ballard, Linda K. Burton, Mzee Ronald A. Rasband, Elaine S. Dalton, Rosemary M. Wixom, na Askofu Gary E. Stevenson wanajadili baraka za kuwa na ukuhani katika kila nyumba.