Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi
Maagano ya Hekalu
Soma kwa maombi na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe. Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye www.reliefsociety.lds.org.
Maagizo ya wokovu yanayopokelewa katika hekalu siku moja ambayo yatatuwezesha kurejea kwa Baba yetu wa Mbinguni katika uhusiano wa kifamilia ya milele na kuimarishwa na baraka na nguvu kutoka juu zinastahili kila kujitolea na kila bidii,1 alisema Rais Thomas S. Monson Kama bado haujaenda hekaluni, unaweza kujitayarisha kupokea maagizo matakatifu ya hekalu kwa:
-
Kuamini katika Baba wa Mbinguni, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu.
-
Kukuza ushuhuda wa Upatanisho wa Yesu Kristo na urejesho wa injili.
-
Kuunga mkono na kufuata nabii aliyehai.
-
Kufuzu kwa kupokea sifu ya hekalu kwa kulipa zaka, kuwa msafi kimaadili, kuwa mwaminifu, kutii Neno la Hekima, na kuishi kulingana na mafundisho ya Kanisa.
-
Kutoa muda, talanta, na mali ili kusaidia kujenga Ufalme wa Bwana.
-
Kushiriki katika kazi ya historia ya familia.2
Rais Monson alifundisha zaidi, “Tunapokumbuka maagano tunayofanya katika [hekalu], tutaweza zaidi kustahimili kila jaribio na kushinda kila jaribu.”3
Kutoka kwa Maandiko
Kutoka kwa Historia Yetu
“Zaidi ya Watakatifu 5,000 walijaza Hekalu la Nauvoo baada ya kuwekwa wakfu. …
“Uwezo, nguvu na baraka za maagizo ya hekalu [zinawahimili] Watakatifu wa Siku za Mwisho wakati wa safari yao [Magharibi], wakati walipo [pitia] baridi, joto, njaa, umaskini, magonjwa, ajali na kifo.”4
Kama wengi wa akina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, Sarah Rich alihudumu kama mfanyikazi wa hekalu. Alizungumzia uzoefu wake: Kama haingekuwa ni imani na maarifa ambayo tulipata katika hekalu hilo na Roho wa Bwana, safari yetu ingekuwa kama moja achukuaye hatua gizani. Lakini tulikuwa na imani katika Baba yetu wa Mbinguni, tukihisi kuwa sisi tulikuwa watu Wake wateule … , na badala ya huzuni, tulihisi kufurahia kwamba siku ya ukombozi wetu imekuja.”5
Safari ya kutoka haikuwa “hatua gizani” kwa wanawake waaminifu wa Watakatifu wa Siku za Mwisho walihimiliwa na maagizo yao ya hekalu.