Maswali na Majibu ya Hekalu
Kwa nini tuna mahekalu?
Mahekalu ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni mahali patakatifu ambapo sisi hujifunza ukweli wa kushughulika katika maagizo matakatifu.
Ndani ya hekalu kuko vipi?
Hekalu ni mahali pa amani, pa heshima, na parembo. Kila kitu ndani ya hekalu ni kisafi na katika utaratibu mzuri. Kila mtu huvalia nguo nyeupe na huongea kwa sauti tulivu.
Nini hufanyika hekaluni?
Mke anaweza kufunganishwa kwa mumewe, na watoto wanaweza kufunganishwa kwa wazazi wao. Kufunganishwa huko huwezesha familia kuwa pamoja kwa milele. Katika hekalu, wanaume na wanawake pia hupokea kipawa cha baraka za kiroho kiitwacho endaumenti. Wanaweza pia kupokea endaumenti na kufunganishwa kwa wale ambao walikufa bila kufanya maagano ya hekaluni.
Nini kingine hufanyika katika mahekalu?
Licha ya kufunganisha na endaumenti, maagizo mengine hukufanyika mahekaluni. Watu wanaweza kubatizwa na kuithibitishwa kwa niaba ya wale ambao hawakuwa na uwezo wa kujiunga na Kanisa walipokuwa hai. Unapofika umri wa miaka 12 na unastahili kuingia hekaluni, unaweza kuwa na nafasi ya kubatizwa na kuthibitishwa kwa niaba ya wale ambao walikufa bila Injili.
Je, na kama familia yangu haijawahi kwenda hekaluni?
Baba wa Mbinguni anakujua na kukupenda wewe na familia yako. Anataka kila mtu kuwa na baraka ya maagizo ya hekaluni. Ishi kustahili kuingia hekaluni. Weka lengo sasa kwamba utapokea endaumenti na kuoa katika hekalu siku moja. Baba Yako wa Mbinguni atakubariki wewe na familia yako.