2013
Ninaweza Kupata Jarida kama Hili Wapi?
Aprili 2013


Ninaweza Kupata Jarida kama Hii Wapi?

Sharon Rather, Nevada, USA

Nilipokuwa katika safari na familia yangu kutoka Nevada, Marekani, kuelekea Alaska, Marekani, nilianzisha mazungumzo na mwanamke mrefu, mrembo, wa kirafiki katika njia baina ya viti.

Aliniuliza nilikokuwa nikienda, na nikamuambia tulikuwa tukielekea Juneau, Alaska, kumtembelea bi wetu na familia yake. Aliniambia kuwa alikuwa ametoka Las Vegas. Kisha, kwa hisia, akaongeza kuwa alikuwa anaenda Juneau kuwatembelea wakwe zake ili kuwa na ushiriki wa kumbukumbu kwa ajili ya mumewe, ambaye alikuwa ameoana naye kwa miaka 20. Alikuwa ameaga hivi karibuni kutokana na saratani.

Niliangalia chini ya njia pana na kujiwazia jinsi nilikuwa na bahati kujua mpango wa wokovu na kuwa mhudumu wa hekalu katika Hekalu la Las Vegas Nevada. Nilijiuliza ni nini ningefanyia mwanamke huyu ili kuinua nafsi yake.

Ghafla, kwa uwazi kama kengele, nilikumbuka nukuu na Rais Joseph Smith niliyokuwa nimepeana katika Muungano wa Usaidizi wa kina mama. Alipoanzisha Muungano wa Usaidizi wa kina mama, aliashiria kuwa kina dada “watapaa hadi kwa usaidizi wa mgeni; watamwaga mafuta na divai katika moyo uliojeruhiwa wa waliogandamizwa; watapanguza machozi ya mayatima na kufanya moyo wa mjane kuwa na furaha” (Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 452).

Niliangalia katika njia pana mara nyingine. Nilimuona mgeni katika dhiki, mjane na moyo uliojeruhiwa. Nilikumbuka kuwa nilikuwa nimesoma Ensign ya Julai 2012 mapema siku hiyo. Ilikuwa na baadhi ya makala ya kuvutia ambayo nilidhani yangempa moyo na faraja.

Nilijipatia ujasiri wangu, nikafungua jarida kwa makala, na kumuliza asome. Nilimuangalia kwa karibu na nikashangaa kuwa alisoma kila mstari—kwa makini. Alipokuwa amemaliza, alisoma makala mengine.

Kwa dhahiri kitu alichokuwa amesoma kilimgusa moyoni. Alilikumbatia jarida kwa nguvu kifuani mwake na kisha akapanguza chozi machoni mwake.

“Ninaweza kupata Jarida kama Hili wapi?” aliniuliza. Nilimuambia kuwa angebaki nalo. Kisha akasoma zaidi.

Tulipofika Juneau, alishika mkono wangu, akaniangalia machoni, na kusema, “Asante.”

Nilijifunza funzo kuu kutoka kwa uzoefu huo. Tumezungukwa na wageni walio na mioyo iliyojeruhiwa wanaohitaji neno jema la kuwafariji na ambao wanahitaji kujua kile ambacho sisi Watakatifu wa Siku za Mwisho tunajua.