“Tunazungumza Kumhusu Kristo,” Liahona, Machi 2024.
Kwa ajili ya Wazazi
Tunazungumza Kumhusu Kristo
Wapendwa Wazazi,
Nefi aliwafundisha watu wake jinsi ilivyo muhimu kumweka Bwana katika sehemu ya mbele kabisa ya maisha yetu. Aliandika, “Tunazungumza kumhusu Kristo, tunafurahia katika Kristo, tunahubiri kuhusu Kristo, tunatoa unabii kumhusu Kristo, na tunaandika kulingana na unabii wetu, ili watoto wetu wajue asili ya kutegemea msamaha wa dhambi zao” (2 Nefi 25:26). Ungeweza kurejea upya mada zifuatazo pamoja na familia yako na watu wengine unaowapenda ili kuwaonesha kwenye injili ya Yesu Kristo, kwenye mwongozo Wake, na kwenye kanuni za hekima ambazo zitatusaidia tumtafute Yeye katika ulimwengu wa kisasa, wenye shughuli nyingi.
Mijadala ya Injili
Injili ya Yesu Kristo ni kwa ajili ya Kila Mmoja
Watu wote wanahitaji tumaini na ukombozi unaotolewa na injili na Upatanisho wa Yesu Kristo. Jadiliana na familia yako baadhi ya mafundisho kutoka kwenye makala ya Mzee Jeffrey R. Holland juu ya jinsi unavyoweza kupenda, kushiriki, na kumwalika mtu fulani aipokee na kuikumbatia injili ya Yesu Kristo (ona ukurasa wa nne).
Kanuni za Hekima kwa ajili ya Matumizi ya Vyombo vya Habari
Teknolojia na vyombo vya habari ni vifaa vyenye msaada wakati vinapotumika kwa usahihi. Rejelea baadhi ya kanuni kwenye ukurasa wa 22 na jadili viwango vya familia yako kwenye matumizi ya vyombo vya habari. Kwa kutumia “maswali ya kutafakari,” fikiria kile kinachokwenda vyema na nini kingeweza kuboreshwa.
Kumfuata Mwokozi katika Imani
Katika makala hii kwenye ukurasa wa 40, Mzee Benjamin M. Z. Tai anashiriki njia nne ambazo kwazo Mwokozi anatusaidia sisi. Baada ya kurejea upya njia hizi pamoja na familia yako, jadili jinsi ulivyosaidiwa kadiri ulivyomfuata Mwokozi katika Imani.
Kutoka Gazeti la Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Toleo la mwezi huu ni maalumu likiwa na dhima “Yesu Kristo ni Nguvu ya Vijana.”
Soma ujumbe kutoka kwa Mzee Jeffrey R. Holland kuhusu jinsi kila kijana anavyoweza kupata nguvu katika Yesu Kristo.
Tafuta makala kuhusu jinsi Mwokozi anavyotuimarisha dhidi ya mfadhaiko, huzuni, dhambi, aibu, udhaifu, mambo ya ulimwengu, na wasiwasi, vile vile makala kuhusu jinsi Yeye ananvyotuimarisha kuhusu kujiandaa na kustahili kuwa wa mahala fulani.
Furahia mabango ya kuvutia na kazi za sanaa juu ya Mwokozi.
Kutoka Gazeti la Rafiki
Pasaka Njema!
Pata hadithi na shughuli ili kuisaidia familia yako iwe na Pasaka ya maana yenye kiini chake katika Kristo.
Tayari kwa ajili ya Mkutano Mkuu
Je, una shauku ya kuangalia Mkutano Mkuu mwezi ujao? Rafiki ya mwezi huu ina Shughuli kwa ajili ya watoto wako kufanya wakati wanaposikiliza.
Kuwa Salama Mtandaoni
Soma hadithi kuhusu msichana ambaye alihisi Roho Mtakatifu akimshawishi kuacha kuangalia video mbaya. Unaweza kupata nyenzo salama za vyombo vya habari kwenye Friend Churchofjesuschrist.org
Jifunze kutoka Kitabu cha Mormoni
Tafuta shughuli za kila wiki, hadithi za maandiko zilizoelezwa kwa mifano, na mengine zaidi ili kuisaidia familia yako ijifunze maandiko kwa kuburudika.