Misaada ya Kujifunza
13. Nyumba ya Ghorofa katika Nauvoo


13. Nyumba ya Ghorofa katika Nauvoo

Picha
picha 13

Joseph Smith, Mdo, na familia yake walihamia ndani ya Jumba la Ghorofa katika Nauvoo Agosti 1843. Baadaye sehemu iliongezwa kwa upande wa mashariki ya jengo kuu na kuwa jumla ya vyumba 22. Kuanzia Januari 1844, Ebenezer Robinson alisimamia nyumba hii kama hoteli, na Nabii alibakisha vyumba sita kwa ajili ya familia yake. Nyumba ilitumika kwa kiasi fulani kama kituo cha kijamii cha watu wa Nauvoo. Wageni maarufu walipokelewa hapa na Nabii.

Matukio muhimu: Mnamo 27 Juni 1844 Nabii Joseph na kaka yake Hyrum walipigwa risasi na kuuawa huko Carthage, Illinois, na miili yao ililetwa katika nyumba hii kwa ajili ya kuonwa na kutoa heshima za mwisho kabla ya mazishi. Wamezikwa katika kiwanja kidogo cha makaburi ya familia ngʼambo tu ya Mtaa Mkuu, magharibi ya nyumba ya zamani ya magogo ambayo Joseph aliishi wakati alipofika Nauvoo kwa mara ya kwanza. Emma Smith aliishi katika hii Nyumba ya Ghorofa hadi mwaka 1871. Baadaye alihamia katika Nyumba ya Nauvoo, ambamo alifia katika mwaka 1879.

Chapisha