Misaada ya Kujifunza
8. Nyumba ya John Johnson


8. Nyumba ya John Johnson

Picha
picha 8

Nyumba ya John na Alice Johnson ilikuwa katika Hiram, Ohio. Chumba hiki kiko katika orofa ya pili.

Matukio muhimu: Joseph Smith Nabii na mke wake, Emma, waliishi katika nyumba hii. Joseph na Sidney Rigdon walipokea ono la kustaajabisha la madaraja ya utukufu katika uwepo wa wengine kadhaa mnamo 16 Februari 1832 (M&M 76). Nabii Joseph pia alifanya kazi ya Tafsiri ya Joseph Smith ya Biblia (TJS) katika nyumba hii. Mnamo 24 Machi 1832, wakati Joseph na Emma walipokuwa wakiishi hapa, kundi la wahuni waliokengeuka na wapinga-Wamormoni waliwapiga vikali na kuwapaka lami na kisha manyoya Joseph na Sidney.

Chapisha