Misaada ya Kujifunza
17. Kutoka kwenda Magharibi


17. Kutoka kwenda Magharibi

Picha
picha 17

Mwanzo wa kuihama Nauvoo, Illinois, kulipangwa kuwa Machi–Aprili, lakini kwa sababu ya vitisho vya kikundi cha wahuni Rais Brigham Young aliagiza kwamba kutoka kwa Watakatifu kuvuka Mto Mississippi kuanze 4 Februari 1846. Rais Young alibaki nyuma ili kutoa endaumenti kwa Watakatifu na hakuondoka Nauvoo hadi katikati ya Februari.

Matukio muhimu: Kabla ya kifo chake Joseph Smith Nabii alitoa unabii, “Baadhi yenu mtaishi hadi kwenda na kusaidia katika kutengeneza makazi na kujenga miji na kuwaona Watakatifu wakiwa watu wenye nguvu katikati ya Milima ya Rocky.” Takribani Watakatifu 12000 waliondoka Nauvoo kuanzia Februari hadi Septemba 1846. Baada ya Watakatifu kuondoka Winter Quarters na maeneo ya karibu, waliwekwa katika makundi ya makumi, ya hamsini, na mamia, chini ya kinara wa kikundi (M&M 136:3). Katika Septemba 1846 kundi la wahuni wapatao takribani wanaume 800 wakiwa na silaha za mizinga sita waliuzingira Nauvoo. Baada ya mapigano ya siku kadhaa, Watakatifu waliosalia walilazimika kujisalimisha ili kuokoa maisha yao na kupata nafasi ya kuvuka mto. Watu mia tano hadi mia sita wanaume, wanawake na watoto walivuka mto na wakapiga kambi katika kingo za mto huu. Rais Brigham Young alituma kikosi cha uokoaji pamoja na vyakula ili kuwahamisha hawa “Watakatifu maskini.”

Chapisha