Misaada ya Kujifunza
10. Adamu-ondi-Amani


10. Adamu-ondi-Amani

Picha
picha 10

Kusini mwa bonde la Adamu-ondi-Amani, bonde tulivu, zuri lililoko katika Missouri ya kaskazini magharibi karibu na jumuia ya Gallatin.

Matukio muhimu: Miaka mitatu kabla hajafa, Adamu aliwaita wazao wake wenye haki katika bonde hili na akaweka juu yao baraka yake ya mwisho (M&M 107:53–56). Katika mwaka 1838 Adamu-ondi-Amani palikuwa ni mahali pa makazi ya Watakatifu wa Siku za Mwisho kati ya 500 na 1000. Watakatifu waliyahama makazi haya wakati walipofukuzwa Missouri. Kabla ya ujio wa pili wa Kristo katika utukufu Adamu na wazao wake wenye haki, ambao ni pamoja na Watakatifu wa vipindi vyote, watakusanyika tena katika bonde hili ili kukutana na Mwokozi (Dan. 7:9–10, 13–14; M&M 27; 107:53–57; 116).

Chapisha