Misaada ya Kujifunza
4. Mtambo wa Kupiga Chapa wa Grandin na Duka la Uchapaji


4. Mtambo wa Kupiga Chapa wa Grandin na Duka la Uchapaji

picha 4

Ni kiwanda cha kupiga chapa kilichojengwa upya cha Egbert B. Grandin huko Palmyra, New York ndipo mahali ambapo toleo la kwanza la Kitabu cha Mormoni kilichapishwa katika mwaka 1830. Martin Harris aliweka rehani shamba lake na aliuza sehemu yake ili kulipia gharama za kupiga chapa nakala 5000 za Kitabu cha Mormoni. Kupanga herufi za kupiga chapa kulianza katika Agosti 1829, na nakala zilizokamilika zilikuwa tayari 26 Machi 1830.

Tukio muhimu: Martin Harris aliamriwa kutoa mali yake kwa ridhaa yake ili kulipia deni la kupiga chapa Kitabu cha Mormoni (M&M 19:26–35).